Habari za Punde

MAHAKAMA YAFUTA KESI YA MANJI NA WENZAKE YA UHUJUMU UCHUMI, SASA WAPO HURU

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia huru Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji na wenzake wawili waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu uchumi.
Manji na wenzake wameachiwa baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha hati ya kuomba kuondolewa kwa mashitaka dhidi yao kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaki.
Baada ya Wakili waSerikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, kueleza nia hiyo ya DPP, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, aliyekuwa akisikiliza shauri hilo aliliondoa na kuwaachia huru washitakiwa hao.
Manji na wenzake ambao waliletwa Mahakamani hapo wakitokea Mahabusu Gereza la Keko, waliondoka Mahakamani hapo kwa kutumia magari binafsi kurejea makwao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.