Habari za Punde

MIKATABA YA BIMA YA MAYFAIR YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Kamishna Wa bima Tanzania (Tira), Bhagayo Saqware akionesha mikataba ya kiswahili ya bima ya May fair mara baada ya kuzindua mkataba hiyo ambao umeiongezea heshima lugha ya kiswahili hapa nchini uzinduzi huo umefanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa bima ya Mayfair,Sanjay Singh na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Sumaria Group,Jayesh Shash.
Mkurugenzi Mkuu wa bima ya Mayfair,Sanjay Singh akizungumza mara baada ya kuzindua Mikataba ya bima ya Kiswahili hapa nchini ambayo italeta uelewa wa kuelewa vizuri mikataba ya bima wanazokata.
Kamishna wa Bima Tanzania (Tira), Bhagayo Saqware katika akikata utepe wakati wa kuzindua mkataba wa bima wa kiswahili ambao umeiongezea heshima lugha ya kiswahili hapa nchini uzinduzi huo umefanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa bima ya Mayfair,Sanjay Singh na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Sumaria Group,Jayesh Shash.
Kamishna Wa bima Tanzania (Tira), Bhagayo Saqware akizungumza mara baada ya kuzindua mikataba ya bima ya Mayfair mara baada ya kuzidua ambayo imeleta tija kubwa kwa ya matumizi ya Lugha ya Kiswahili pamoja na kukuza Lugha yetu hapa nchini ikiwa ni Mkataba wa Kwanza kuandikwa kwa kiswahili.
Mkurugenzi Mkuu wa Sumaria Group,Jayesh Shash akizungumza mara baada ya kuzindua Mikataba ya kiswahili ya bima ya Mayfair jijini Dar es Salaam ambayo italeta tija kubwa kwa watumiaji wa Bima hiyo hapa nchini.
Waanzilishi wa Bima ya Mayfair wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mikataba ya kiswahili ya bima ya Mayfair jijini Dar es Salaam.
************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog,Dar
KATIKA kiuenzi lugha ya Kiswahili, kampuni ya bima ya Mayfair imezindua mkataba wa bima uliotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ili kumuwezesha mwananchi kuelewa haki zake kwa lugha rahisi anayoielewa moja kwa moja.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kamishna Wa bima Tanzania (Tira), Bhagayo Saqware amesema, mkataba huu wa bima wa kiswahili wa Mayfair umeiongezea heshima lugha ya kiswahili kwani wameonyesha wanaiheshimu lugha ya taifa inayotumiwa na watanzania takribani milioni 50.
"Lugha ya kiswahili inazungumzwa na zaidi ya wazungumzaji milioni 200 kutoka ndani na nje ya Tanzania, mktaba huu utawawezesha kwenda mbele zaidi" amesema Saqware.
Ameongeza kuwa mkataba kwa lugha ya kiswahili utawaongezea wananchi wengi uwezo wa ufahamu wa bima na hivyo kufanya shughuli ya mamlaka ya bima kuelimisha jamii juu ya bima itakuwa imepata msukumo.
Aidha ametoa wito kwa makampuni mengine ya bima kufanyia mabadiliko mikataba yao kama walivyofanya Mayfair kwa kuandaa mikataba kutoka lugha ya kingereza kwenda kiswahili ambayo ni mabadiliko chanya.
Amesema yakijitokeza makampuni mengi kufanya hivyo, yatasaidia kukuza kiswahili kwani mpaka sasa bima ya Mayfair wameingia katika vitabu vya historia vya ndani na nje ya nchi kwa kukuza lugha ya kiswahili.
Ameongeza, kulikuwa na changamoto kubwa, watu wengi walikuwa hawajui haki zao kupitia mikataba ya kiingereza lakini tafsiri hii sasa itawawezesha kujua haki zao ambapo ili kuhamasisha hilo tunatoa tuzo mbali mbali kwa makampuni yanayofanyia mabadiliko mikataba yao kwa kutoa tozo nafuu katika utoaji wa leseni na kuharakisha.
" Ili mtu uelewe jambo lolote, lazima ulipate jambo hilo kwa lugha yakwako* " kama mtu unaweza kuota usiku kwa njia ya kiswahili basi ujue wewe unajua kiswahili na kama haujawahi kuota kwa kiingereza basi hujui kiingereza" amesema.
Naye. Mkurugenzi wa bodi UA myfair, William Erio amesema mkataba huo utawezesha watu wengi kunufaika na Huduma za bima ya Mayfair kwani mtu atakuwa anauhakika yuko salama kwa kuelewa nini kipo ndani ya mkataba, "Kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu nchini vhhapa tumepata mafanikio makubwa, Mayfair ni kampuni ya kwanza katika sekta ya bima Tanzania kutafsiri mkataba wa bima ya magari kwa kiswahili.
Waanzilishi pamoja na wafanyakazi wa Bima ya Mayfair wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Mkataba wa bima hiyo kwa Lugha ya Kiswahili jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.