Habari za Punde

MSANII Ne-Mo KURUDI UPYA NA KIPOTABO SEPT 19

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Shaban Mpute 'Ne-Mo' amesema amedhamiria kurudi rasmi kivingine jukwaani katika muziki, huku akitarajia kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'Kipotabo' Septemba 9 mwaka huu.
Akizungumzia ujio wake huo mpya Ne-Mo 
chini ya lebo ya 'Digital City Drimz' alisema 
kuwa amedhamiria kuirejesha RnB ya Bongo 
katika viwango na pia kuipeleka nje ya 
mipaka ya Tanzania
.
Alisema kwa sasa kuna wasanii kama 
Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, 
Navy Kenzo na wengineo wameubeba muziki 
wa Bongofleva na kusaidia kuupenyeza 
kimataifa, naye ana matumaini makubwa ya 
kufika walipo wasanii hao.
Alisema nyimbo yake hii mpya inayokwenda 
kwa jina la 'Kipotabo' ambayo imetengenezwa 
katika studio za Combination Sound chini ya 
mtayarishaji Man Water,na video 
kutengenezwa na Kwetu Studio.
Ne-mo ujio wake utakuwa wa aina yake na 
Watanzania hawatajutia kumsubiri Ne-Mo 
arudi kwa muda wote huo, kwamba ukimya 
wake umetokana na masomo ambapo 
aliamua kutulia amalizie masomi kisha 
aendelee na Harakati za Muziki. 
Alisema alikuwa masomoni amesomea 'Mass 
Communication' anaeleza kuwa sasa 
ametulia na amepata 'Mameneja ' ambao 
wanamsimamia na kumrejesha kwa kishindo 
katika muziki.
"Nimejipanga vuzri pamoja na mameneja 
wangu narudi kimuziki kikweli kweli, naomba 
mashabiki wa muziki Tanzania wanipokee 
kwa mara nyinyingine, nilitoka kidogo 
kwenda masomini lakini sasa nimerudi rasmi 
katika muziki"alisema Ne-mo.
Alisema kwa upande wa mtindo wa Rap na 
Hip Hop mwanzoni mwa miaka ya 2000 
Profesa Jay alichangia kuuweka muziki wa 
Hip Hop mtaani na kukubalika na kila kundi 
la jamii., miaka michache iliyopita waliibuka 
kina Child Benz na Nako 2 Nako ambao 
walisaidia kujenga misingi ya kuufanya 
muziki wa Hip Hop kukubalika kibiashara. 
Alisema sasa hivi wasanii kama Weusi, 
Darasa, Billnas, Young Dee na kadhalika 
ambao wanauwekea vionjo muziki wa Rap 
kufanya kupenya zaidi na hata uanze 
kuimbwa na hata akina dada ambao zamani 
ilikuwa ni nandra kuwa na mapenzi ma 
muziki wa Rap.
Meneja wa mwanamuziki huyo Habibu Anga 
'Guru Picasso' alisema kuwa siku ya Jumatatu 
wataachia rasmi wimbo wa Kipotabo wa 
msanii huyo.
Alisema Ne-mo alikuja kuitikisa zaidi 
Tanzania na Afrika Mashariki mwaka 2013 
alipoanchia wimbo uliokwenda kwa jina la 
"Number One" ambao alimshirikisha mkali 
mwenzake 'Ommy Dimpoz' wimbo ambao 
ulikuwa mkubwa na kugeuka kama 'wimbo 
wa Taifa' kama wasemavyo mtaani.
Baada ya mafanikio makubwa ya wimbo huu 
wa 'Number One' Ne-Mo hakuwahi kutoa kazi 
yake nyingine yoyote ile, zaidi ya nyimbo za 
kushikishwa ambazo ni 'Mrs Superstar' ya 
Young Killer, 'Tulikuwepo' ya Niki Mbishi,  
'Sijutii' ya Msamiati na nyinginezo nyingi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.