Habari za Punde

MSUVA AWAHENYESHA BOTSWANA APIGA MBILI STARS IKISHINDA 2-0

 Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Simon Msuva, akishangilia bao lake aliloifungia timu yake kipindi cha kwanza, wakati wa mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jioni ya leo. Katika mchezo huo Stars imeshinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Simon Msuva katika dakika ya 5 na 61.
 Beki wa Stars Erasto Nyoni (kulia) akiwania mpira na beki wa Botswana Simisani Mathumo.
*************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
SIMON Msuva leo ameonyesha kile kilichowafanya klabu ya Difaa Hassan El- Jadida ya nchini Morocco, kumsajili baada ya kuibeba timu yake ya Taifa Taifa Stars kwa mabao yake 2-0 dhidi ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Msuva aliyejiunga na timu ya Ligi Kuu ya Morocco mwezi uliopita na huku akiwa tayari ametupia mabao 9 akicheza mechi 11 na kukosa mechi moja, 

leo alikuwa shubili kwa mabeki wa Botswana na kutupia mabao hayo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Elly Sasii aliyesaidiwa na Soud Lila na Frank wote wa Tanzania, hadi mapumziko Taifa Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Simon Msuva alipokea pasi ndefu ya kiungo Hamisi Abdallah wa Sony Sugar ya Kenya, na kuifanyia kazi nzuri na kumpasia kiungo, Muzamil Yassin kabla ya kuiomba tena na kuingia nayo kwenye boksi kwa kasi na kufumua shuti kali lililompita kipa wa Botswana 'The Zebras', Mwambule Masule katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza.
 Kiungo wa Stars, Farid Mussa, akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Botswana, Kabelo Seakanyeng
 Kiungo wa Stars, Farid Mussa, akipiga krosi mbele ya mchezaji wa Botswana, Kabelo Seakanyeng
 Mshambuliaji wa Stars, Elias Maguli, akipambana kuwatoka mabeki wa Botswana, Simisani Mathumo (kulia) na Lopang Masige
 Himid Mao (kulia) akimtoka Katlego Masole, wakati wa mchezo huo
 Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Simon Msuva (kushoto) akimtoka beki wa Botswana, Edwin Olerile, wakati wa mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwewnye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Winga wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Shiza Kichuya, akiwania mpira na beki wa Botswana, Edwin Olerile, wakati wa mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwewnye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta (kushoto) akijaribu kumhadaa beki wa Botswana, Edwin Olerile, wakati wa mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwewnye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Simon Msuva, akipambana kuwania mpira na mchezaji wa Botswana,Simisani Mathumo, wakati wa mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwewnye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Shiza Kichuya, akijaribu kupiga shuti katikati ya mabeki wa Botswana.
*********************************************

Mashambulizi ya Taifa Stars leo ambayo katika benchi la Ufundi imeongezewa nguvu na mchezaji wa zamani, Amy Ninje aliyecheza hadi Uingereza Ligi za Madaraja ya chini na kocha wa zamani wa Azam, Dennis Kitambi ambaye kwa sasa anafundisha AFC Leopards ya Kenya. 
The Zebras nao hawakuwa wanyonge kabisa uwanjani, kwani walipeleka mashambulizi langoni mwa Taifa Stars na kukaribia kufunga mara mbili kama su uhodari wa kipa wa Simba, Aishi Salum Manula.
Kipindi cha pili, Zebras walirudi kwa nguvu na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Taifa Stars, lakini safu ya ulinzi ikiongozwa na mkongwe Kevin Yondan ilikuwa imara kudhibiti hatari zote. 
Hatimaye Msuva akawainua tena vitini mashabiki wa nyumbani kwa kufunga bao la pili dakika ya 63 baada ya kugongeana vizuri na winga wa Simba SC, Shiza Ramadhani Kichuya.
Nahodha, Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji alicheza vizuri pamoja na kudhibitiwa vikali na akakaribia kufunga mara mbili – unaweza kusema bahati haikuwa ya kwake leo. 
Kiungo wa Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa Dhofar ya Oman wote waliingia kipindi cha pili na wakacheza vizuri sawa na chipukizi, Emmanuel Martin wa Yanga aliyempokea Msuva.
Kikosi cha Tanzania:

 Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Abdi Banda, Kevin Yondan, Himid Mao, Simon Msuva/Emmanuel Martin dk82, Hamisi Abdallah/Said Ndemla dk80, Muzamil Yassin/Raphael Daudi dk57, Mbwana Samatta/Elias Maguri dk82 na Shiza Kichuya/Farid Mussa dk66.

Kikosi cha Botswana: Mwambule Masule, Mosha Gaolaolwe/Jackson Lesole dk74, Edwin Olerile/Tmisang Orebonye7 dk4, Simisami Mathumo, Lopang Mogise, Alphonce Modisaotsile, Maano Ditshupo/Katlego Masole dk70, Gift Moyo, Segolame Boy, Kabelo Seakanyeng na Ontireste Ramatlhakwana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.