Habari za Punde

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM-TAIFA JIJINI DAR

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam.

***************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi, imepitisha majina ya wagombea nafasi za uenyekiti wa CCM wilaya, huku wagombea kutoka wilaya nne wakienguliwa.
Imeelezwa kuwa kuenguliwa kwa wilaya hizo, kumetokana na kasoro za kimaadili zenye viashiria hatarishi kwa chama.
Wilaya ambazo wagombea wameenguliwa hadi pale uchaguzi utakapotangazwa tena ni Moshi Mjini, Siha, Hai zote za mkoani Kilimanjaro na Makete, mkoani Iringa.
Pia uchaguzi kwenye wilaya ya Musoma utatangazwa baadaye mara baada ya Halmashauri Kuu kuamua kuundwa kwa wilaya mpya mbili za kichama, ambazo ni Musoma Mjini na Musoma Vijijini.
Akizungumza kuhusu uamuzi huo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alisema katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika jana, Ikulu Dar es Salaam, wagombea zaidi ya 1,400 walijadiliwa.
Alisema wagombea waliopitishwa kushiriki uchaguzi huo wanapaswa kuzingatia kanuni za uchaguzi, uongozi, maadili na katiba ya CCM.
Polepole alisema wagombea watakashindwa kuzingatia maadili, chama kitawachukulwa hatua, ikiwemo kuwafukuza uanachama.
“Kama ikibainika kuwepo kwa rushwa, chama hakitakuwa na ajizi kufuta uchaguzi huo, ikiwemo wahusika kufukuzwa uanachama.
“Yeyote atakayeshinda uchaguzi kwa rushwa, atayang’anywa ushindi na kuvuliwa uongozi,” alisisitiza.
Katibu huyo wa Itikadi, alieleza kuwa wagombea waliopitishwa kuwania nafasi hiyo wanapaswa kuzingatia msisitizo wa chama wa nafasi mmoja kwa mtu mmoja.
Alisema kwa wagombea watakaokuwa na nafasi mbili mara baada ya uchaguzi huo, wanapaswa kuachia nafasi mmoja.
Alisema uvumi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari hauna ukweli kwani Kinana amekuwa akitekeleza majukumu yake, ikiwemo kushiriki vikao vya Sekretarieti vilivyofanyika Dodoma hivi karibuni.
Orodha ya majina ya wagombea waliopitishwa na halmashauri kuu kuwania nafasi za uwenyekiti wa CCM kwenye wilaya mbalimbali nchini.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe. Dkt. John Magufuli akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Rodrick Mpogolo kabla ya kufungua mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)   jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam. 

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiendelea na Kikao jijini Dar es Salaam. 
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiendelea na Kikao jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.