Habari za Punde

NAIBU SPIKA ATOA ZAWADI YA PIKIPIKI NA PESA TASLIMU KWA WASHINDI WA TAMASHA LA TULIA TRADITIONAL FESTIVAL 2017

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia) akimkabidhi funguo ya Pikipiki Kiongozi wa Kundi la Ngoma la Kannengwa Rungwe, Nolbert Mwandinga, baada ya kundi lake kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Ingoma Kituli, wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki. 
 Dkt. Tulia akikabidhi zawadi ya Pikipiki
 Kiongozi wa kundi la ngoma akishangilia ushindi  akiwa haamini kama ameitwa kukabidhia Pikipiki

1.  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akipata elimu kuhusu mafao yanayotolewa na PPF kutoka kwa  Meneja Uhusiano wa  Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, alipotembelea banda la PPF katika  Tamasha la ngoma za asili (Tulia Traditional Dances Festival 2017),  lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Mbeya

1.  Mwananchi akipata maelezo kuhusu kuchangia na kupata taarifa mbali mbali kupitia simu ya mkononi,ambapo PPF imerahisisha huduma zake kwa wanachama pindi anapokuwa amejiunga kupitia mfumo wa Wote scheme anaweza akachangia popote pale alipo. Kulia ni mfanyakazi wa PPF akitoa maelezo
Wacheza Bao Gabriel Mwasankinga wa timu ya CCM (kushoto) akichuana na Pascal Mbwelembweta wa timu ya Kawechele, kutafuta mshindi wa tatu katika mchezo wa fainali za mchezo huo kuadhimisha Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
  Wacheza Bao Kocha Lufingo wa timu ya Stendi Kuu (kushoto) akichuana na Six Willson wa timu ya Soko Kuu, kutafuta mshindi wa kwanza na wapili katika mchezo wa fainali za mchezo huo kuadhimisha Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.Katika mchezo huo Six Willson (kushoto) alishinda. 
Mchuano ukiendelea
 Wamasai wakiburudiasha kwa ngoma yao...
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akicheza ngoma ya asili ya kundi la  Banyampulo ya kabila la Wanyakyusa, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
 Zawadi ya Pikipiki 
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipokea michango ya hela kutoka kwa wananchi wa Tukuyu kwa ajili ya harambee ya kuichangia timu ya Tukuyu Stars ''Changia Tukuyu Stars irudi Ligi Kuu'' wakati wa  Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
 Mabalozi wa Tulia Trust, Babra Hassan Ditto wakichangia mfuko wa Tukuyu Stars
 Dkt. Tulia akipokea zawadi kutoka kwa adau
 Kina mama wakimvisha shuka Dkt Tulia
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimkabidhi cheti cha Udhamini Meneja Uhusiano wa  Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, kwa kutambua mchango wa kufanikisha na kuwa wadhamini wa Tamasha la ngoma za asili (Tulia Traditional Dances Festival 2017), lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Mbeya. Ambapo pamoja na udhamini huo Mfuko wa Pensheni wa PPF ulitumia nafasi hiyo kutoa elimu na kuandikisha wanachama wapya kwa sekta isiyokuwa rasmi kupitia Mfumo wao wa Wote Scheme ambapo baadhi ya washiriki waliweza kujiunga na  Mfuko wa PPF.
 Mwakilishi wa Vodacom akipkea Cheti
 TCRA wakipokea Cheti kama sehemu ya wadhamini wa Tamasha hilo
Dkt. Tulia akiwa kaka picha ya pamoja na mabalozi wake

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.