Habari za Punde

NYUMBA YA MBUNGE ZITTO KABWE YATEKETEA KWA MOTO KIGOMA

Nyumba ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliyoijenga wakati akigombea ubunge kwa mara ya kwanza iliyopo Kibingo, Kata ya Mwandiga Kigoma mjini ikiungua moto ambao haikuweza kufahamika chanzo chake kwa haraka.
Msaidizi wa mbunge huyo, Nyembo Mustafa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hata hivyo Zitto hakuwa anaishi kwenye nyumba hiyo.
Amesema Zitto alihama kwenye nyumba hiyo baada ya kujenga nyumba nyingine kubwa kwenye kiwanja hicho hicho na hiyo iliyoungua ilikuwa ikitumika kwa dharura.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.