Habari za Punde

RUTAINURWA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA JUMUIA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA

Na Bashir Nkoromo, Dar
Lucas Rutainurwa ametawazwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana.
Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo, amesema katika Uchaguzi huo uliofanyika Segerea, Rutainurwa (pichani), alipata kura 278 dhidi ya Mohamed Honelo aliyepata kura 148 baada ya hao wawili kuingia katika kinyang'anyiro kwa mara ya pili kufuatia kutopatikana mshindi aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa awali.
Wakati katika awamu ya kwanza Lutainurwa alipata kura 277 Honelo alipata kura 243 huku Celestine Nyalusi akipata kura 67.
Nafasi ya Mjumbe wa Halimashauri Kuu aliyeshinda ni George MJtambalike ambaye amepata kura 195 dhidi ya Edward Haule aliyepata kura 181.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.