Habari za Punde

SIMBA WAKANUSHA OMOG KUPEWA MECHI TANO WAWATAKA MASHABIKI WAO KUTULIA

Na Devotha Kiwhelo, Dar
UONGOZI wa Klabu ya Simba leo umejitokeza hadharani na kukanusha taarifa zinazoenezwa kuwa Kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog amepewa mechi tano za kujitathimini bila kupotezana kuwataka mashabiki wao kuzipuuza taarifa hizo. 
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Klabu ya Simba iliyopo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam,Ofisa habari wa Simba Hajji Manara, amesema Kaimu Rais wa timu hiyo, Salim Abdallah amezungumza na kocha Omog na kumueleza kuwa afanye anachoona kinawezekana katika kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika Ligi Kuu bara na michezo ya kimataifa kwa mwaka huu. 
Aidha Manara amesema uongozi  na kamati tendaji unamuamini kocha huyo huku wakiwataka mashabiki kumuacha kocha afanye kazi yake na kuacha kutunga maneno ambayo si kauli za viongozi wa klabu hiyo.
 "Kumekuwa na tabia ya mashabiki kufurahia timu inaposhinda mechi zake na kuona ni timu yao lakini timu inapofanya vibaya wanamsukumia kocha na kuzusha kwenye mitandao mbalimbali kwa kusingizia uongozi umesema ili watugombanishe na benchi la ufundi", alisema Manara. 
Mbali na hilo Manara amedai kuwa kwa sasa hawapo tayari kumfukuza kocha kwa kuwa wamejifunza kubadilisha makocha kila mara sio sababu ya kupata ushindi bali ni kujiweka pabaya zaidi. 
Kuhusu mechi ya Simba na Mbao timu inatarajia kuondoka kesho alfajiri na kuweka wazi kuwa watakosa huduma ya wachezaji wao wawili akiwepo Said Mohamed 'Nduda' ambaye anaenda India kwa matibabu na Shomari Kapombe ambaye ataanza mazoezi wiki hii.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.