Habari za Punde

STARTIMES TANZANIA KUFUNGUA SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA SAUTI.Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, David Kisaka akitoa ufafanuzi kuhusu shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania kwa watanzania kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu yake yaliyopo jijini Beijing nchini China.
*************************************

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar.


STARTIMES Tanzania kupitia chaneli yake ya Star Swahili kufungua pazia jipya la shindano la kusaka vipaji vya sauti litakalofanyika jijini la Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro amesema mashindano hayo ni fursa tosha kwa washiriki pamoja na ajira kwa washiki pamoja na washindi hao. 
Amesema kuwa shindano la kusaka vipaji vya sauti litakalofanyika katika maeneo matatu hapa nchini ambayo ni jiji la Dar es Salaam watachukua washindi kumi, jijini Mwanza watachukua washindi watano na Zanzibar watachukua washindi watano hao wote wataingia fainali itakayohusisha washiriki 20. 
Washindi wa Shindano la kusaka vipaji vya sauti watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya Startimes yaliyopo jijini Beijing nchini China.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi amesema kuwa Startimes Tanzania wanasaidia kukuza vipaji vya vijana pamoja na kukuza kiswahili ndani na nje ya Tanzania. 
Amewaasa Startimes kuangalia namna ya wasanii hao kunufaika na kazi zao mara baada ya kumaliza mikataba. Pia alisisitiza kuwepo namna ya kunufaika kati ya nchi mbili ambazo ni Tanzania na Chini katika kazi hizo za sanaa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi akizungumza kwenye mkutano wa kwanza kati ya Startimes Tanzania pamoja na waandishi wa habari unaohusu shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya Startimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania.
Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro akizungumza na waandishi wa habari na wageni mbalimbali kwenye awamu ya kwanza ya kuandaa shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania litakalofanyika Dar Es Salaam, Mwanza na Zanzibar.
Mhadhiri kutoka Taasisi ta Taaluma za Kiswahili(UDSM), George Mrikaria akizungumza kuhusu chuo hicho kitavyoweza kwenda sambamba na Startimes ili kuweza kuwapata washindi wazuri watakaoitangaza pamoja na kukitangaza kiswahili katika nchi mbalimbali hasa nchini China.
Baadhi ya Waandishi wa habari pamoja wageni mbalimbali wakiangalia moja ya dokumentari ya washindi kumi walioshinda kwenye shindano la kusaka vipaji vya sauti lililoandaliwa na kampuni ya StarTimes Tanzania na kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya Startimes yaliyopo jijini Beijing nchini China .
Meneja Masoko na Maudhui, Li Kun(kulia) pamoja na Msimamizi wa Shughuri za Startimes Tanzania, Pauline Kaka wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea katika mkutano wa kwanza kati ya Startimes Tanzania pamoja na waandishi wa habari unaohusu shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya StarTimes.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatialia awamu ya kwanza ya uzinduzi wa shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya Startimes Tanzania kupitia chaneli yake ya Star Swahili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.