Habari za Punde

TANZIA : MSIBA WA MSANII MOHAMED IDD MTURUMA AKA MUDDY ALEYKUWA ANAISHI UJERUMANI AMEFIA NCHINI SPAIN

Msanii Marehemu Mohamedi Idi Mturuma aka Muddy
*********************************
Umoja wa Wa Watanzania Ujerumani kwa ushirikiano na watanzania wanaoishi England na Spain kwa masikitiko makubwa sana tulipata msiba wa ndugu yetu mtanzania mwenzetu mcheza sarakasi Mohamed Idi Mturuma aliekuwa akiishi koloni Ujerumani na kufariki nchini spain alikokwenda kikazi. Aliaga dunia tarehe 19.09.17 Kwa ushirikiano wa Watanzania wanaoishi nchi hizo tumeazimia kufanya kila liwezekanalo ili kuweza kusafisrisha mwili wa Marehemu ndugu yetu Mohamed Idi Mturuma kwenda kuzikwa nyumbani Tanzania Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU.e.V ) Unawatangazia watanzania wote wanaoishi popote pale Duniani kuunga mkono azma yetu kwa kutoa michango ya hali na mali ili tumsafirishe mwenzetu.
Shukran nyingi kwa msanii Mussa FAB Moses Kutoka England ambaye alisafiri mara baada ya msiba kutokea kwenda Spain kwa ajili ya kusaidia mchakato wa kuandaa kusafirisha mwili wa marehemu. Mussa Fab Moses anategemea kusafiri na mwili wa Merehem kwenda Tanzania kwa Mazishi.
Watanzania wanaoishi England mnaweza kuwasiliana moja kwa moja na Saidi Kanda ili kuwasilisha michango yenu namba ya kiganjani +447404066607

Watanzania wanaoishi Tanzania mnaweza kuwasiliana na Eddy Sengo ili kuwasilisha michango yenu namba ya kiganjani +255656210725

Watanzania wanaoishi Ujerumani mnaweza kuwasiliana na Makamo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTUe.V) Malumbo Salim Malumbo namba ya simu +49 1522 4082848
Mwili wa Marehemu ulisaliwa msikitini siku ya ijumaa iliyopita tarehe 22.09.17 na kupelekewa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya kusubiria safari. UMOJA NI NGUVU; PENYENIA PANA NJIA; TUKITAKA TUTAWEZA KWA KUDRAZA MWENYEZIMUNGU INSHALLAH
WABILAHI TAWFIQ
UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU e.V)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.