Habari za Punde

TRL KUSITISHA SAFARI ZAKE KWA SAA 48 KUKARABATI DARAJA LA MOROGORO NA MAZIMBU

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Reli Tanzania (TRL), Focus Makoye, akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) wakati akitangaza kusitishwa kwa safari za Kampuni hiyo kwa saa 48 kwa ajili ya kufanya marekebisho ya uboreshaji wa Miundombinu ya Reli eneo la Kati la stesheni ya Morogoro na Mazimbu katika Daraja lililoharibika kutokana na mvua kubwa mvua zilizonyesha hivi karibuni. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu waMasoko, Shaaban Kiko (kushoto) ni Kaimu MKuu wa Usalama wa Reli na Ulinzi, Mhandisi Adolphina Ndyetabula. 
Baadhi ya waandishi wa habari katika mkutano huo.
*****************************************
Na Ripota wa Mfoto Blog, Dar
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) inatarajia kufanya marekebisho ya miundombinu katika kituo cha stesheni ya  Morogoro na Mazimbu  ambapo jumla ya abiria 4000 watakosa huduma ya usafiri kwa saa 48.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi  wa  TRL, Focus Makoye, alisema  sababu ya kufanya ukarabati  huo ni kutokana na daraja lililopo eneo hilo lenye urefu wa kilometa 209.7 kuharibika kwa mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Makoye alisema uongozi  umeona ni muda muafaka wa kulifanyia marekebisho ili  kuhakikisha usalama wa wateja  na wananchi wanaotumia usafiri huo.
Alisema ili kazi hiyo iweze kufanyika kwa ufanisi na umakini, kampuni imefanya marekebisho ya ratiba za safari  kwa lengo la kulitengeneza daraja hilo katika  hali ya ubora.
"Treni yetu  ya abiria ya siku ya Jumanne ya Septemba 19,mwaka huu ya kutoka Dar es Salaam  kwenda Mwanza na Kigoma  na  treni ya Alhamisi ya Septemb 21 ya kutoka  Kigoma  na Mwanza kuja Dar es Salaam  tumezifuta  na hazitakuwepo kwa muda wa saa 48,"alisema.
Aidha Makoye, alisema  ratiba  nyingine za usafiri zitabaki kama  zilivyo kawaida hadi watakapotangaza na kuwaomba radhi wananchi kwa usumbufu utakaojitokeza na kuwataka kuwaunga mkono  ili kuweza kuendeleza  kutoa huduma za uhakika na usalama zinazostahili.
Kwa upande wa Kaimu  Meneja wa Masoko  TRL, Shaban Kiko,  alisema kutokana na  maboresho hayo utaisababishia kampuni  kukosa mapato ya siku mbili japo si muhimu kwao zaidi ya usalama wa abiria wao.
"Mbali na ukosefu wa mapato tunachokiangalia zaidi kwetu ni   usalama wa abiria wetu na huduma kuwa bora,"alisema Kiko
Mhandisi wa TRL,Adolfina Ndyetabula,alisema watafunga  barabara hiyo kwa saa 48  ili kupisha mashine kuweza kufanya kazi kwa uharaka.
"Tukifanya  kazi bila kusimama itatusaidia kuepusha uhatarishi wa mizigo, hivyo  tunawaomba   radhi  abiria wetu kwa usumbufu  utakaojitokea  kwa kipindi hicho kifupi," alisema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.