Habari za Punde

TUME YA MUFTI YAKABITHI RIPOTI YAKE KWA WAZIRI LUKUVI

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akimsisitiza kufuatilia kwa makini maeneo yote ya waislam yanayomilikiwa na BAKWATA na yaliyomilikishwa watu kinyume cha utaratibu yanatafutiwa ufumbuzi kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akimkabidhi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi Ripoti ya Tume ya Mufti ofisini kwa Waziri. 
Ujumbe wa Tume ya Mufti ukiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi ofisini kwake.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akiongozana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi baada ya kumkabidhi Ripoti ya Tume ya Mufti.
***********************************
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amekutana na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir pamoja ujumbe wake wa Tume ya Mufti iliyoundwa kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA zinar ejeshwa.
Waziri Lukuvi amepokea ripoti hiyo ikiwa ni kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli la kumtaka Waziri Ardhi afuatilie kwa makini maeneo yote ya waislam yanayomilikiwa na BAKWATA na yaliyomilikiswa watu kinyume cha utaratibu yanatafutiwa ufumbuzi.
Katika ujumbe huu Mufti ameongozana na Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA Mwalimu Salim Abeid, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Ally Ngeruko, Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mufti na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Issa Othman Issa na Katibu wa Tume ya Mufti Alhaj Omary Igge.
Baada ya kukabithi ripoti hii Mufti Sheikh Abubakar Zubeir amemshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kupokea Ujumbe wake wa Tume ya Mufti na kumuomba achunguze na kuchambua kwa makini maeneo yote ya Bakwata yanayohusiana na migogoro ya ardhi.
Tume hii ya Mufti ya Kuhusu urejeshaji wa mali za waislam iliundwa na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir mara baada ya kukukutana Mheshimiwa Rais na kumuomba awasaidie kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA zinarejeshwa BAKWATA.
Mara baada ya kupokea ripoti hii Waziri Lukuvi amemuahidi Mufti Sheikh Abubakar Zubeir kwamba atatekeleza agizo hilo la Mheshimiwa Rais na ataifanya kazi hii katika muda mfupi ujao na kusimamia kikamilifu kwa kufuata sheria.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.