Habari za Punde

BAADA KUPATA SARE YA SITA MAYANGA AWATUPIA LAWAMA WASHAMBULIAJI


Na Ripota wa Mafoto Blog,Dar
BAADA ya kupata sare ya sita tangu achukue mikoba ya Boniphace Mkwasa, kocha wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Salum Mayanga amesema safu yake ya ushambualiaji ilikosa umakini wa kutumia nafasi.
Stars ililazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Malawi mwishoni mwa wiki katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Timu ya Taifa ya Malawi ilianza kupata bao katika dakika ya 35 kupitia kwa nahodha wao, Robert Ng'ambi ambapo Stars ilizawazisha dakika ya  59 kufuatia Saimon Msuva aliyechonga kona moja kwa moja iliyozama katika nyavu.
Stars ilikosa nafasi za wazi katika dakika za 57, 59, 67 na 87 kufuati kwa washambuliaji wake Mbwana Samatta, Mbaraka Yussuf na Saimon Msuva aliyekosa katika dakika ya 23 na 55.
Akizungumza baada ya mchezao huo, Mayanga alisema kikosi chake kilikosa umakini wa kutumia nafasi za wazi waliziopata.
Alisema sababu kubwa iliyofanya kupata sare hiyo ni kutokana na washambuliaji wake kutokuwa makini katika kutumia nafasi.
Mayanga alisema ana kazi kubwa ya kukaa na safu yake ya washambuliaji ili kuinoa jinsi ya kuwa makini na nafasi.
Alisema mpira wa miguu ni mchezo wa makosa hivyo walifanya makosa kukosa nafasi nyingi za wazi ambazo zimewagharimu kupata sare.
"Mkosa yetu yametugharimu, haikutakiwa tupate sare, tumecheza vyema na tumetengeneza nafasi za wazi lakini tumekosa umakini wa kufunga," alisema Mayanga.
Kocha huyo anayetarajia kuita kikosi kitakachocheza mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Uganda hivi karibuni, alisema atahakikisha anatatua changamoto za kikosi chake kabla ya mchezo huo kufika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.