Habari za Punde

DIAMOND AGAWA VIFAA TIBA NA ZAWADI HOSPITALI YA AMANA DAR

Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akimsalimia mtoto wa Mama Nadia Iddi ambaye amejifungua katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam ambapo msanii huyo alifika kuwatembelea watoto waliozaliwa hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya kuhadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Meneja wa Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond), Said Fellaakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufika katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kutoa msaada wa Vifaa tiba.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa ameongozana na Mtangazaji wa kipindi cha leo Tena Dahuu kwenda kutoa msaada katika hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond), akisalimiana na Mmoja ya wamama aliyopo na mtoto wake katika wodi ya watoto ya Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa katika maeneo ya Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva , Naseeb Abdul (Diamond) akiwa na Mtangazaji wa kipindi cha leo tena cha Clouds Fm Dahuu wakati alipowasili katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.