Habari za Punde

KESI YA DAWA ZA KULEVYA YA MASOGANGE YASOGEZWA MBELE


Video Qeen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa mashtaka ya matumizi ya Dawa za kulevya na ambapo kesi yake imepigwa kalenda hadi Novemba 14, 2017.
******************************************


Tima Sikilo, Dar
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imesogeza mbele kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mrembo wa Video za muziki (Video Qeen), Agnes Gerald, maarufu kama Masogange hadi Novemba 14 mwaka huu ambapo shahidi wa upande wa utetezi atatoa ushahidi wake.
Mshtakiwa Masogange alitakiwa kuanza kutoa utetezi wake hii leo lakini wakili wa Serikali, Adolf Mkini, ameiomba Mahakama ya Hakimu Kisutu kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine.
Masogange ataanza kujitetea baada ya Mahakama kumkuta na kesi ya kujibu baada ya upande wa mashtaka kuleta mashahidi watatu na ambapo pia, Masogange, anatarajia kuita mashahidi watatu.
Inadaiwa kuwa Masogange mnamo Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Aidha anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.