Habari za Punde

BAADA YA JANA MAYANJA KUJIUZULU LEO SIMBA YATAMBULISHA, MRITHI WAKE KUTOKA RWANDA

Kocha mpya msaidizi wa Klabu ya Simba, Masoud Djuma, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitambulishwa baada ya utangazwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Kocha msaidizi Jackson Mayanja, aliyetangaza kujiuzulu nafasi hiyo jana. Kushoto kwake ni Msemaji wa Simba, Haji Manara.
Ofisa Habari wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara, akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Klabu hiyo, wakati akimtambulisha Kocha mpya wa Klabu hiyo Masoud Juma, kutoka timu ya Lyon ya Rwanda aliyefika kuchukua nafasi ya Kocha msaidizi Jackson Mayanja, aliyetangaza kujiuzulu nafasi hiyo jana. Kulia ni Kocha Msadidi mpya wa Simba aliyetambulishwa, Masoud Djuma.
Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, akifurahia jambo na Kocha Mpya Msaidizi wa Klabu hiyo, Masoud Djuma, wakati wa hafla fupi ya kutambulishwa iliyofanyika kwenye Ofisi za Klabu hiyo zilizopo Msimbazi jijini Dar es Salaam, leo mchana.
********************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
UONGOZI wa klabu ya Simba leo mchana umemtambulisha kocha mpya atakayevaa viatu vya aliyekuwa kocha msaidizi Jackson Mayanja pamoja na meneja mpya anayechukua nafasi ya Dr Cosmas Kapinga.
Akitoa utambulisho huo mbele ya waandishi wa habari, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa Kocha Masoud Djuma kutoka Rayon Sports ya nchini Rwanda na kocha bora wa msimu uliopita kupitia klabu hiyo anakuja kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyeachia ngazi kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia nchini Uganda.
Manara amesema kuwa, kabla ya kufikia makubaliano ya kuachana na Mayanja tayari walikuwa wameshaanza mazungumzo na kocha Djuma kuja kusaidiana na kocha Jospeh Omog kuinoa klabu hiyo.
Akizungumza baada ya kutambulishwa Kocha Djuma, amesema kuwa amekuja Simba kusaidiana na kocha Omog kuwezesha kupata mataji mbalimbali na sio kufanya maajabu kama watu watakavyodhani.
“Sijaja kufanya maajabu, nimekuja kuisaidia Simba kwa kidogo nilichonacho ili kuisogeza mbele zaidi ”, alisema Djuma huku akiweka wazi zaidi kuwa amekuja kufanya kazi na falsafa yake ni kocha mwenye pande mbili mkali na mpole lakini huwa mkali pale ambapo mchezaji anataka kuharibu kazi.
Kocha Masoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulisha na afisa wa habari wa Simba Haji Manara (Kulia) akichukua nafasi ya Jackson Mayanja aliyejiuzulu jana.
************************************
“Mimi ni mtu wa pande mbili kwa ufupi ni kama kiganja cha mkono, kina pande mbili. upande mmoja mpole lakini kwa upande mwingine ni mkali. Nimekuja hapa kufanya kazi ili kuipeleka Simba mbele na mimi nisogee mbele.”amesema Djuma.
Kuelekea mechi ya watani wa jadi Okotoba 28, Djuma ameweka wazi kuwa toka amezaliwa ameanza kusikia Simba na Yanga kwahiyo anazijua vizuri , “Nimezaliwa nimekuwa nazisikia Simba na Yanga, kila sehemu kuna mechi zenye presha kubwa siwezi kuahidi lolote kuhusu mechi ya Simba na Yanga kwa sababu mpira una matokeo matatu.”

Ili kuliboresha benchi la ufundi, Klabu ya Simba imemtambulisha meneja anayerirhi mikoba ya Cosmas Kapinga, Richard Robert mwenye uzoefu wa masuala ya mpira na utawala ambapo awali aliwahi kuwa meneja wa wanja wa ndege na pia katika kituo cha JKM Park.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.