Habari za Punde

KUELEKEA SHINDANO LA MISS UNIVERSE KESHO JUMAMOSI, LEO WAREMBO WATEMBELEA TATEDO

   Warembo wanaowania taji la Miss Universe Tanzania 2017, wakiwa katika picha ya pamoja Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi ((kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali la (TaTedo) Jensen Shuma na Mwakilishi  kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Martha Ngolowela mara baada ya kutembelea ofisi hizo na kujifunzo ujuzi mbalimbali wa kujiajiriamali.
Mmoja wa wataalum wa Shirika Lisilo la Kiserikali la TaTedo Eva John aliwaelezea washiriki wa mashindano ya Miss Universe Tanzania jinsi ya kutumia jiko la kisasa la kuoka keki
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO)Jensen Shuma akielezea warembo wa Miss Universe Tanzania jinsi ya kutengeneza mkaa kwa kutumia pumba na mabaki mbalimbali. Anayefuatilia maelezo hayo ni Mtaalam wa Nishati Endelevu na mabadiko ya Tabia nchi  Shima Sango.
Mmoja wa warembo wa Miss Universe Tanzania akitengeneza jiko la kisasa la udongo na bati mara baada ya kupata maelekezo na mmoja wa wataalam wa Taasisi ya Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO)
******************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Mashindano ya kumsaka mrembo wa Kiss Universe Tanzania yamepangwa kufanyika leo (Jumamos) kwenye ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa jijini.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 10 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa mujibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi.
Maria amewataja mabondia hao kuwa ni Lilian Maraule , Glory Gideon, Melody Tryphone, Anitha Mlay, Silvia Mkomwa, Rogathe Ally, Prisca Dastan ambao wote wanatoka Dar es Salaam.
Warembo wengine ni Maureen Foster na Mary Peter wanaotoka Mwanza wakati anayetoka mkoa wa Mbeya Zahra Abdul. Warembo hao walipata mafunzo mbalimbali katika kambi ikiwa pamoja na mafundisho ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Jensen Shuma.
Warembo hao walipata ujuzi wa jinsi ya kutengeneza majiko ya kisasa ya kupikia kwa kutumia udongo na bati, jinsi ya kutengeneza majiko ya kuoka keki yenye gharama nafuu, jinsi ya kutengeneza mkaa kwa kutumia pumba mbalimbali na ujuzi mwingine.
Maria alisema kuwa walipata mafunzo hayo kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais upande wa Mazingira  ili kuwawezesha warembo kupata ufahamu na kuhamasika kujiajiri ili kujipatia kipato.
 “Maandalizi ya mashindano  hayo yamekamilika na wapenzi wa masuala ya urembo watapata burudani safi kutoka kwa  DDI Dance, poetry group (Romantic), A beautiful song kutoka kwa Jeff  Mduma,” alisema Maria.
Alifafanua kuwa wamedhamilia kumpata mrembo bora ambaye atarejesha heshima ya mashindano hayo kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata ambaye alimaliza katika nafasi tano bora nchini Mexico mwaka 2007.
“Tumefanya uchaguzi wa warembo vizuri na wengi ni bora, kwa sasa tunawafundisha masuala mbalimbali ya urembo, lengo ni kuwafanya wawe bora, wote ni washindi, lakini tunahitaji mshindi mmoja ambaye ataliwakilisha Taifa katika mashindano ya Kimataifa,” alisema.
Alisema kuwa mashindano hayo pia yatamtoa mshindi wa taji la Miss Earth Tanzania na mshindi wa taji la Miss Tourism Queen International wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.