Habari za Punde

LIGI YA SOKA LA UFUKWENI KUANZA MWEZI JANUARI MWAKANI

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Salum Madadi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza kuanza rasmi kwa Ligi ya Soka la Ufukweni 'Beach Soccer' inayotarajia kuanza mwezi Januari mwakani. Kushoto ni Mwakilishi wa Kampuni ya SHADAKA, Edgar Kibwana (kulia) ni Mratibu wa Beach Soccer Tanzania, Deo Lucas.
*****************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeandaa bonanza la siku moja la michuano ya Sola la ufukwenu (Beach Soccer) ambalo linaratibiwa na Kampuni ya michezo ya SHADAKA likitarajia kufanyika Oktoba 14, mwaka huu katika Ufukwe Escape One, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwenye Ofisi za TFF leo mchana, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi, amesema bonanza hilo litakuwa na lengo la kuwakutanisha wadau kwa ajili ya kujadili Ligi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Januari mwakani.
Alisema bonanza hilo litasaidia kupata timu mbalimbali zitakazochuana katika ligi hiyo.
Aidha Madadi amesema kuwa bonanza hilo litahusisha kuanzia timu kumi hadi 12 ambapo bingwa wa hatopata zawadi yeyote.
Hata hivyo, Madadi amezitaka timu kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata usajili wa kucheza ligi itakayoanza Januari mwakani na kuwataka wadau kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kudhamini mchezo huo unaokuja kwa kasi nchini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.