Habari za Punde

MACHUPA AREJEA BONGO KUKIPIGA MCHANGANI

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
IMEKUWA ni kawaida kwa wachezaji wazawa wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi baada ya kumalizana na timu zao kuamua kurejea nchini, kama ambavyo amefanya mshambuliaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Athumani Machupa, sambaye asa amerejea nchini kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Machupa ambaye alikuwa akicheza soka ya kulipwa nchini Sweden anatarajia kuanza mazoezi hivi karibuni na kikosi cha Friends Rangers ambacho kinashiriki Ligi Daraja la kwanza FDL msimu huu.
Akizungumza na Ripota wa Mafoto Blog, jijini Dar es Salaam, Machupa amesema ameamua urejea nchini kwa kuwa soka la nje limeshaanza kumtupa mkono kutokana na ushindani wa vijana chipukizi uliopo kwa sasa.
Alisema amecheza soka la kulipwa nchini Sweden zaidi ya miaka mitatu hivyo ushindani uliopo Ulaya unampa wakati mgumu kuzidi kung'ara na kuonyesha uwezo kama aliokuwa nao wakati akitua nchini humo.
“Nimeangalia kasi yangu niliyokuwa nayo Ulaya, kule ni soka la ushindani zaidi ya Tanzania hivyo kwa miaka inavyoendelea kusonga nimeona bora nirudi nyumbani kwa kuwa kasi nayo inapungua," alisema Machupa.
“Nataka kuisaidia Friends Rangers kwa sababu ndio klabu iliyonilea tangu nikiwa mdogo, nilianza kuonekana nikiwa pale kabla ya kujulikana sehemu yoyote. Kwa hiyo mimi kurudi Rangers ni sehemu ya kuisaidia klabu yangu kutokana na uzoefu nilionao wa ndani na nje ya nchi kuhakikisha timu inafanya vizuri na kupanda ligi kuu”. amesema
Mkongwe huyo wa kupasia kamba amesema hajafikiria kuingia kwenye ukocha kwa sababu tayari Friends Rangers wamepanga kumsaidia mchezaji wao wa zamani Jabir Aziz kusomea ukocha ili baadae aisadie timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.