Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TAASISI YA WORLD WOMEN'S BANKING

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan, akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker kufungua Mkutano Mkuu wa siku tatu wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali 'World Women's Banking' ulioanza Dar es Salaam, leo kwa lengo la kujadili na kufikia malengo ya kusaidia Wanawake Ulimwenguni ili kufikia Maendeleo ya Wanawake. Mkutano huo unafanyika Afrika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Washiriki wa mkutano huo
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo
 Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Shine Dance Tz, Michael Mtopwa, akibinjuka sarakasi mbele ya washiriki wa Mkutano mkuu wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali 'World Women's Banking' ulioanza Dar es Salaam, leo kwa lengo la kujadili na kufikia malengo ya kusaidia Wanawake Ulimwenguni ili kufikia Maendeleo ya Wanawake. Mkutano huo unafanyika Afrika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Shine Dance Tz, Sanaa Arts Kijitonyama wakitoa burudani katika mkutano huo.
 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha 
 Picha ya pamoja
 Picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB baada ya kufunguliwa mkutano huo.
MAKAMU wa Rais, Samia Hassan Suluhu, amesema ni muhimu wanawake kushirikishwa ipasavyo katika sekta za kifedha ili kuchochea kukua kwa uchumi duniani.
Amesema katika hatua hiyo Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele kwa wanawake katika sekta za kifedha ikiwemo kuwapa upendeleo wenye uwezo wa kushinda tenda nyingi ili kuwawezesha kufikia uchumi wa kati.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika Mkutano Mkuu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Benki ya wanawake ya Duniani,  ulioandaliwa na Benki ya NMB, Samia amesema ni lazima kuhakikisha wanawake wanafikiwa na huduma ipasavyo ili kuwawezesha kushiriki katika sekta za kifedha.
Alisema katika kufikia hali hiyo nchini ni muhimu kutumia fursa ya matumizi ya huduma za kifedha katika mitandao ya simu itakayowezesha  kuwaunganisha na huduma za benki.
“Ipo haja ushirikiano uliopo baina ya taasisi za kifedha ikiwemo benki na mitandao ya simu kuboreshwa ili wanawake wanaotumia huduma hiyo waweze kuunganishwa ipasavyo huku pia benki zikitafuta namna ya kuwafikia wanawake wengi zaidi hususani wa vijijini,”amesema.
Samia alisisitiza haja ya Benki ya NMB kuendelea kutoa huduma zinazowagusa moja kwa moja wanawake ikiwemo miradi ya watoto, vikundi na mikopo nafuu na  kuwaunganisha katika biashara.
Alisema imefika wakati wa kuhakikisha washiriki katika mkutano huo wanafikia lengo la kujadili maendeleo ya wanawake kwa kina na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia maendeleo ya wanawake ulimwenguni.
“Katika hali hiyo ni muhimu kushirikisha sekta binafsi Tanzania tunaendelea kupiga hatua ambapo idadi ya wanawake wanaoshiriki katika sekta za kifedha ni kiashiria cha kuwapo na utekelezaji wa mpango kazi wa malengo ya maendeleo endelevu  SDG’s,”amesema.
Mpango huo unaungwa mkono na Rais Dk. John Magufuli kuwezesha wanawake nchini kwa kuwapa kipaumbele katika haki ya msingi ikiwamo elimu ya msingi na sekondari kwa watoto wa kike.
Alisisitiza haja ya Benki ya Wanawake nchini kuhakikisha wanaongeza matawi vijijini na kuwafikia watu wengi zaidi kwa kushusha riba za mikopo kuweza kuchochea uchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa NMB Abdulmajid Nsekela alisema washiriki zaidi ya 300 duniani wameshiriki katika mkutano huo unaofanyika nchini ambao kwa Nchi za Afrika ni mara yake ya kwanza.
Alisema watahakikisha katika mkutano huo wanajadili mbinu za kuwafikia wanawake wa chini na kuwawezesha  kufikia huduma za kifedha.

“Tunafahamu kuweza kufikia mipango mikakati ya kiuchumi nchini ni lazima kuwezesha wanawake katika kilimo,biashara,vikundi vidogovidogo na sekta nyingine kwa kuwahusisha katika teknolojia za huduma za kifedha ili kuwainua kiuchumi na kukuza pato la Taifa,”amesema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.