Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, IRELAND NA MOROCCO KWA NYAKATI TOFAUTI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa kutoka kwa Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam.
****************************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock, Ikulu jijini Dar Es Salaam.
Balozi alizungumzia masuala mbalimbali yakiwemo kuwawezesha wanawake katika nafasi za kisiasa, Masuala ya Mimba za utotoni na namna ya kukabiliana na vifo wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliiomba nchi ya Ireland kuendelea kusaidia Tanzania katika kutoa elimu ya uzazi ili kupunguza Vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua.
Wakati huo huo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amkutana na kuzungumza na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane mwenye makazi yake mjini Nairobi,Kenya.
Katika mazungumzo yao, Balozi wa Morocco alimpatia taarifa ya utekelezaji wa yote yaliokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco na kumueleza Makamu kwamba utekelezaji wa mambo hayo umefikia hatua nzuri.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpongeza Balozi kwa kusimamia utekelezaji huo ndani ya muda mfupi.
Makamu wa Rais alimueleza Balozi huyo wa Morocco kuwa uhusiano uliopo kati ya nchi mbili hizi ni wa kudumu na utasaidia katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika nchi hizi.
Mwisho Kabisa Makamu wa Rais alikutana na kuzungumza na Balozi wa Sausi Arabia Mhe. Mohammed Almalik .

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.