Habari za Punde

MANJI SASA HURU MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YAKE

 Mfanyabiashara Yusufu Manji akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo akiongozana na baadhi ya wadau wake baada ya Mahakama kumwachia huru upande wa Mashitaka uliposhindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yake.
****************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Mfanyabiashara Yussuf Manji ameachiwa huru leo baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yake za kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.
Hukumu hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo upande wa jamhuri  ulikuwa na mashahidi watatu huku Manji akileta mashahidi saba.
Alisema katika kufikia maamuzi mahakama hiyo ilibidi iangalie mbali na sheria na masuala ya kitaalamu ya kisayansi na kemia.
Alisema jukumu la kudhibitisha mashitaka pasi kuacha shaka ni la upande wa jamhuri, lakini mshitakiwa ndiye aliyeleta wataalamu akiwepo Profesa Janabi kutoka taasisi ya moyo ya jakaya kikwete.
"Nimeona hakuma sababu ya kumtia hatiani mshitakiwa, hivyo namuachia huru," alisema hakimu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.