Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiambatana na Binti yake katika matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti yaliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
Meza
kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu watatu kutoka kushoto wakati alipofungua matembezi ya hisani
ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, kulia kwa Mh. Waziri ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage na
kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Grace
Maghembe.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimkabidhi cheti moja ya wadau waliofanikisha matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti iliofanyika mapema leo katika viunga vya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakirusha Maputo juu kuashiria ufunguzi rasmi wa matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, iliofanyika katika viunga vya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.
Wadau kutoka taasisi mbali mbali walioungana na Mh. Ummy Mwalimu na watumishi wa Hospitali ya Ocean Road katika matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti yaliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
*******************************************
Na WAMJWW
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu aagiza Hospitali, na Vituo vya Afya vyote vya Serikali nchini
kuanzia leo October 26 kutoa huduma ya uchunguzi wa Saratani kila siku wakati
wa kliniki ya mama na mtoto, sambamba na huduma hizi, kila mwezi vyatakiwa kuwa
na siku moja kwaajili ya kuchunguza na kufanya matibabu ya ugonjwa wa saratani ya
mlango wa kizazi na saratani ya matiti.
Ameyasema hayo wakati alipofungua matembezi ya hisani ya
kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, yalifunguliwa katika viwanja vya hospitali ya Ocean Road
mapema leo jijini Dar es salaam.
Aidha Mh. Ummy ameipongeza kazi nzuri inayofanywa na Uongozi
wa Hospitali ya Ocean Road katika kutimiza majukumu yake ikiwemo kuongeza vitanda
40 mpaka vitanda 100 kwa gharama zao kwaajili ya wagonjwa wa
saratani pindi wanapopata huduma za matibabu ya Chemotherapy.
“Katika kuwaunga mkono Serikali ya awamu ya tano ya Mh.
Magufuli imewapatia Bilioni 5 kwajili yakukamilisha mashine za kisasa za
matibabu ya Saratani kwa kutumia mionzi.” Alisema Mh. Ummy Mwalimu
Aidha Mh. Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa Uongozi wa
Hospitali ya Ocean Road kuwa wanatakiwa kwenda kwenye shule za Msingi na
Sekondari ili kuwajengea watoto uelewa kuhusu ugonjwa wa Saratani, lakini ni vipi wataweza kujikinga na magonjwa
yasiyo yakuambulizwa ikiwemo ugonjwa wa Saratani.
Pia Mh. Ummy alitoa rai kwa wananchi wote hususani wanawake
kujitokeza kupima ugonjwa huo kwani unatibika endapo itagunduliwa mapema,
Nae Mganga Mkuu wa
Mkoa Dkt Grace Maghembe ambae pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam ,
ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Dkt. John Pombe Magufuli
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto kwa kazi
kubwa wanayoifanya ikiwemo kuongeza kwa bajeti ya Dawa , vifaa tiba vya
uchunguzi na matibabu.
Kwa upande mwingine Dkt. Grace Maghembe kwa niaba ya bodi
ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa
uaminifu na bidii kubwa katika kuhakikisha kwamba wanakabiliana na
ugonjwa huu wa Saratani kwa wananchi hasa wale wa hali ya chini na kuahidi
kuendelea kuboresha huduma hii.
“Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kwenda kupima Saratani
kwani ni bure, usisubiri mpaka kuugua, ukichelewa grarama zinaongezeka lakini
pia uwezekano wa kupona unakuwa ni mdogo”. Alisema Dkt Grace Maghembe
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dkt.
Julius Mwaiselage amemhakikishia Mh. Ummy Mwalimu kwamba upatikanaji wa dawa
katika Hospitali hiyo ni 80% na dawa za wagonjwa wengi zinapatikana kwa 100%, ukilinganisha
na 2015/2016 upatikanaji wa dawa ilikuwa
4% tu, jambo ambalo lilikuwa ni
changamoto kubwa na kufanya malalamiko ya dawa kuwa makubwa sana katika
hospitali hiyo, hivyo kuishukuru Serikali ya Magufuli kwa niaba ya Waziri wa
Afya Mh. Ummy Mwalimu.
Mwisho Dkt. Julius Mwaiselage amemhakikishia Mh. Waziri
kwamba Hospitali ya Ocean Road ipo katika hatua ya Mwisho ya kuweka mashine
mpya mbili (Linear accerelators), hivyo zitasaidia kupunguza muda wa kusubiri kwa
wagonjwa kusubiri huduma , lakini kubwa kupunguza wagonjwa wanaokwenda kutibiwa
nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment