Habari za Punde

MISS UNIVERSE AIOMBA JAMII KUSAIDIA KUTATU TATIZO LA UGONJWA WA MDOMO SUNGURA
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa 
midomo sungura wakati wa siku ya 
"Smile day" kwenye hospitali ya CCBRT ya 
jijini Dar es Salaam, leo .Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa 
Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans na Mama mzazi wa mtoto huyo.


**************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Miss Universe Tanzania ambayo uandaliwa na kampuni ya Compass Communications chini ya mkurugenzi, Maria Sarungi Tsehai, Jihan Dimachk ameiomba jamii kusaidia watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa midomo sungura (Mdomo wazi) kupata matibabu yanayofaa.


Jihan alisema hayo wa maadhimisho ya "Smile day" katika hospitali ya CCBRT ya jijin kwa kushirikiana taasisi ya Smile Train Africa linalojishughulisha na utatuzi wa tatizo la mdomo sungura.


Jihan ambaye ni balozi wa shirika hilo alisema kuwa jamii inatakiwa kuwakubali na kushirikiana katika kutatua tatizo hilo ambao linawaathiri sana watoto wadogo.


Alisema kuwa taasisi ya Smile Train Africa linatambua tatizo la ugonjwa huo kwa watoto ambao ukosa raha katika kula na kufanya mambo mengine muhimu.


"Nimefarijika sana kuwa balozi wa Taasisi ya Smile Train Africa na hasa katika kuondoa tatizo la ugonjwa wa Mdomo Sungura, naomba Jamii iunge mkono juhudi za taasisi hii kwani jukumu letu sisi,"


"Ugonjwa huu upo mikoa mingi na watoto wanahitaji msaada wa kufanyiwa upasuaji na gharama za matibabu na gharama ni kubwa, nimeguswa sana na tatizo hili, " alisema.


Taasisi ya Smile Train Afrika hutoa msaada wa kifedha na vifaa ili kusaidia kufidia gharama kwa ajili ya upasuaji. Uwekezaji wote huu si tu kwamba unawezesha upasuaji mkubwa lakini pia unafanya upasuaji huu uwe salama na wa ubora wa hali ya juu.
Mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa 
ugonjwa wa midomo sungura wakati wa siku ya 
"Smile day" akishiriki katika siku hiyo. 
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na 
wazazi na watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa 
ugonjwa wa midomo sungura. 
Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na 
wafanyakazi wa hospitali ya CCBRT wakati wa 
siku ya "Smile day" iliyofanyikia kwenye 
hospitali hiyo.


Miss Universe Tanzania, Jihan Dimachk akiwa na  mmoja wa watoto alyetibiwa na kupona ugonjwa  wa ugonjwa wa midomo sungura. Kulia ni mmoja wa  

wafanyakazi wa hospitali ya CCBRT Brenda Msangi. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.