Habari za Punde

MSAGA SUMU, AMBER LULU, BARNABA KUNOGESHA SHINDANO LA MISS VYUO VIKUU KESHO

 Warembo wa Vyuo Vikuu wakiwa katika mazoezi Ukumbi wa Maisha Club kujiandaa na shindano linalofanyika kesho Ukumbi wa King Solomon, uliopo Namanga, jijini Dar es Salaam.
****************************
Na Ripota wa Mafoto, Blog

Dar es Salaam. Wanamuziki nyota wa muziki bongo fleva, Barnaba Classic na mwanadada nyota, Amber Lulu watapamba mashindano ya kumsaka mrembo wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” yaliyopangwa kufanyika leo Ijumaa kwenye ukumbi wa King Solomoni.
Mbali ya wakali hao wa muziki wa Bongo Fleva, pia mkali wa miondoko ya Singeli, Msaga Sumu naye atafanya ‘vitu vyake’ katika shindano hilo litakalaoshorikisha juml ya warembo 15 kutka vyuo mbalimbali jijini. Pia atakuwepo mchekeshaji maarufu, JK Comedian.
Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya Glamour Bridal Tanzania baada ya kupewa idhini ya waandaaji wa Miss Tanzania, Lino International Agency kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).
Mkurugenzi wa Glamour Bridal Tanzania Muba Saedo alisema kuwa pia kutakuwa na wageni waalikwa ambao ni Basila Mwanukuzi na Irene Uwoya.
“ Maandalizi yamekamilisha, warembo wote wapo vizuri, mbali ya burudani ya wasanii nyota wa Bongo Fleva, pia warembo nao watatoa burudani yao kuanzia shoo ya ufunguzi na mpaka mwisho, hii inatokana na mafunzo mazuri kutoka kwa wakufunzi wao Clara Michael na ba matron, Blessing Ngowi,” alisema Saedo.
Mbali ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), mashindano hayo yatashirikisha vyuo vya Taasisi ya Uhasaibu Dar es Salaam (TIA), IFM, CBE, UDOM, Tumaini – Makumira na Taasisi ya Uhasibu wa Arusha (IAA) na Chuo Kikuu Cha Ardhi.
Saedo alivitaja vyuo vingine kuwa ni Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Tanzania Aviation University College na Magogoni

Warembo wa Vyuo Vikuu wakiwa katika mazoezi Ukumbi wa Maisha Club kujiandaa na shindano linalofanyika kesho Ukumbi wa King Solomon, uliopo Namanga, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.