Habari za Punde

NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA SUMATRA

  Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Bw. Gilliard W. Ngewe (kulia) akimueleza Mhe. Naibu waziri jinsi mfumo wa VTS unavyofanya kazi
Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia sekta za Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta J. Nditiye jana alifanya ziara yake Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) kwa mara ya kwanza. Katika ziara hiyo yenye lengo la kujitambulisha na kufahamu shughuli zinazofanywa na Mamlaka hii alifanya kikao na Uongozi wa SUMATRA na kutoa salam na miongozo mbalimbali.

Salam za Pongezi kwa SUMATRA
Katika kikao chake na uongozi wa Mamlaka, Mhe. Nditiye alitoa salam za pongezi kwa Mamlaka kwa utendaji wa kazi kwa uadilifu na uweledi unaozingatia kanuni na sheria za utumishi wa umma.
‘Sijawahi kisikia kashfa ya SUMATRA kukosa uadilifu au kuhusu mapato ya Serikali, labda kuhusu kazi zenu za udhibiti ambazo kwa kawaida mkifanya kazi zenu vizuri ni lazima mtalaumiwa, tunashukuru ajali zimepungua,
endeleeni kufanya kazi kwa uadilifu na ueledi, tunaomba sana uadilifu uendelee ili mapato ya Serikali yaonekane’ alisema 

Aidha Mhe. Nditiye alisisitiza kuwa Serikali haitakuwa tayari kuona mtu yeyote akiikwamisha katika kuwahudumia wananchi hivyo wafanyakazi wote wa SUMATRA wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kanuni na sheria za utumishi wa umma.
 Ziara ya VTS
Baada ya mkutano wake na uongozi wa SUMATRA, Mhe. Nditiye alitembelea Kituo cha Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi Yanayofanya Safari za Mikoani (VTS) kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Akiwa kituoni hapo Mhe. Nditiye alikiri kuwa mfumo wa VTS ni mzuri na kama Serikali, wanajua kuwa wamiliki wa mabasi hawapendi mabasi yao yapinduke, hivyo ni muhimu kuwa na uwazi na ushirikishwaji wa wamiliki wa mabasi (TABOA) katika ufungaji wa vifaa vya VTS. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.