Habari za Punde

NAIBU WAZIRI SHONZA AFANYA ZIARA TCRA

 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (kulia) alipofanya ziara TCRA kuangalia namna taasisi hiyo inavyosimamia maudhui ya vyombo vya habari nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (katikati) akizungumza alipomtembeza Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kuangalia gari lililofungwa mtambo wa kusimamia masafa ya redio nchini wakati wa ziara yake TCRA leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Posta TCRA Bibi. Cecilia Mkoba (kulia) akimuelezea Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) namna mawasiliano zamani yalivyokuwa yakifikishwa kutoka eneo moja kwenda eneo lingine alipotembelea makumbusho ya mawasiliano leo wakati wa ziara yake TCRA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) alipotembelea Idara inayosimamia maudhui ya televisheni zote nchini wakati wa ziara yake TCRA leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akizungumza na menejimenti ya TCRA alipofanya ziara katika Taasisi hiyo kuangalia namna inavyosimamia maudhui ya vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba. Picha na: Genofeva Matemu -WHUSM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.