Habari za Punde

NANI KUCHEKA, NANI KULIA OKT 28?

KUELEKEA katika mchezo wa watani wa Jadi, Yanga na Simba, Oktoba 28 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Jumamosi hii, rekodi zinaonyesha kumbeba kocha wa Simba, Joseph Omog katika mchezo huo.
Omog ambaye alichukua mikoba ya Jackson Mayanja kukinoa kikosi hicho Agosti mwaka jana, amekuwa na rekodi nzuri kila anapokutana na George Lwandamina katika mechi zao.
Omog na Lwandamina hadi sasa wameshakutana mara nne ambapo mara tatu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na moja ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika Zanziba kila mwaka.
Katika mechi zote hizo Joseph Omog anamatokeo mazuri dhidi ya Lwandamina, ameshinda mechi zote tatu walizokutana (mechi mbili kwa penati) na mchezo mmoja ameshinda ndani ya dakika 90.
Simba ya Omog ilianza na sare ya 0-0 dhidi ya Yanga ya Lwandamina katika michuano ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika January 10, mwaka huu Zanzibar ambapo Simba iliibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalti na kuitoa Yanga katika Nusu fainali.
Mara ya pili walikutana Februari 25, mwaka jana ambapo Simba iliibuka na ushindi wa 2-1. Magoli yalifungwa na Shiza Kichuya na Laudit Mavugo huku Simon Msuva alifunga goli la Yanga kwa mkwaju wa penati.
Pambano la tatu kati ya Omog na Lwandamina ilikuwa Agosti 23, mwaka huu  mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo Simba walishinda kwa penati baada ya mechi kumalizika bila timu zote kufungana ndani ya dakika 90. Simba walishinda kwa penalti 5-4.
Kwa takwimu hizo, inaonekana Lwandamina ni kibonde wa Omog kila wanapokutana katika kichuano mbalimbali hivyo Omog ataingia katika mchezo huo akibebwa na rekodi hizo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.