Habari za Punde

SAMATTA NI JINA HATARI SANA MALAWI: NAHODHA ROBERT NG'AMBI

 Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar 
NAHODHA wa timu ya Taifa ya Malawi, Robert Ng'ambi amesema kabla wahawacheza na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' waliambiwa wamkabili Mbwana Samatta.
Ngambi ambaye nduye mfungaji wa bao la Malawi, alisema benchi lao la ufundi lilikuwa likimhofia nahodha wa Tanzania, Samatta.
Alisema walipewa mazoezi maalumu ya kumkaba Samatta ambapo kocha wa kikosi chao alihitaji mabeki wake wanne wawe makini na Samatta.
Ngambi alisema kocha wao alitumia muda mwingi kuwapa mbinu za kumkabili Samatta kuliko kufundisha mbinu za kupata mabao.
Alisema aliposikia taarifa za nahodha huyo wa Taiofa Stars anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji alianza kumhofia.
"Kila mtu alikuwa akimhofia Samatta, benchi la ufundi lilikuwa likituambia tumkabe sana yeye kwa kuwa ndio siri ya ushindi wa Tanzania," alisema nahodha huyo.
Hata hivyo alisema haikuwa kazi rahisi kumzuia straika huyo mahiri asicheke na nyavu kwa kuwa ana mbinu nyingi miguuni mwake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.