Habari za Punde

SERIKALI YAINGIZA SH. M 15 MAKATO YA KODI FEDHA ZA WASHINDI WA BAHATI

MSEMAJI wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi YA Sh. Milioni 84, mshindi wa droo ya Perfect 12, Japhet Wilson (kushoto) baada ya kubashiriki michezo 12 kiusahihi. Wapili (kulia) ni Msafiri Mtupili ambaye pia ni mshindi wa droo hiyo na mwakilishi wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Sadik Elimsu.
**************************************
*Washindi wanne,wazawadiwa Sh milioni 21 kila mmoja
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
SERIKALI imeingiza Sh. milioni 15 ikiwa ni makato yaliyotokana na fedha walizolipwa washindi wa mchezo wa kubahatisha wa M-Bet. Fedha hizo jumla ya Sh. milioni 84, zimetolewa na Kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya M-Bet na kuwazawadia washindi wanne waliotabiri kwa usahihi katika mchezo wa Perfect 12, ambapo kila mshindi amejipatia jumla ya Sh. milioni 21.
Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa M-Bet, David Malley aliwataja washindi hao kuwa ni Msafiri Mtupili, Pius Damas, Japhet Wilson  na Shame Mwinyi.
“Huu ni mwendelezo wa kampuni yetu katika kuwawezesha watanzania wanaobashiri mchezo wetu wa Perfet 12 ambao kwa sasa unazidi kushika kasi, lengo la M-Bet ni kuona wanaoshiriki katika kubashiri wanapata kile kinachostahili bila ya matatizo yeyote,” alisema Malley.
Aidha alisema droo ya kuwapata washindi hao ilifanyika Oktoba 25 na kila mshindi aliweka dau la Sh 1,000 ambayo imemwezesha kupata kiasi kikubwa cha fedha.
Mmoja wa washindi hao, Msafiri Mtupili alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ni mtaji katika maisha yake na sasa anauwezo wa kujenga nyumba.
“Mimi kwetu ni Utete mkoani Morogoro, sikutarajia kupata kiasi hiki cha fedha, ebu fikiria nimecheza sh 1,000 na kujishindia kiasi kikubwa cha fedha, hii ni faraja sana kwangu,” alisema Mtupili.
Mwakilishi wa Kampuni ya michezo wa kubahatisha nchini, Sadiki Elimsu aliipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwazawadia washindi mbalimbali na kuwawezesha kimaisha.
“Nawaasha vijana, waachane na masuala ya kutumia fedha kwa ajili ya ulevi, ni fursa kucheza kwa kiasi kidogo na kujishindia kiasi kikubwa cha fedha, huu ni wakati wa kubadilika na kushiriki katika michezo hii ya kubahatisha,” alisema Elimsu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.