Habari za Punde

SHEKH PONDA AJISALIMISHA POLISI

Katibu mkuu wa Baraza la mashirika ya kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central kufuatia agizo la kamanda mkuu wa polisi wa Kanda maalum Dar es Salaam RPC Lazaro Mambosasa.
Kiongozi huyo wa dini aliwasili kituo cha polisi leo asubuhi akiwa na wakili wake Abdallah Safari.
Mambosasa siku ya Alhamisi alimwagiza Sheikh Ponda kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kutokana na matamshi ya uchochezi aliyoyatoa.
Kulingana na kamanda huyo , Kiongozi huyo wa dini alifanya makosa hayo siku ya Jumatano wakati wa mkutano na vyombo vya habari na alitakiwa kujisalimisha kati ya Alhamisi na Jumamosi la sivyo akamatwe.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.