Habari za Punde

SHINDANO LA MISS UNIVERSE TANZANIA KUFANYIKA JUMAMOSI HII, KUMTOA MISS UTALII

Mashindano ya kumsaka mrembo wa Miss Universe Tanzania yamepangwa kufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini, Dar es Salaam.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 10 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi.
Maria amewataja warembo hao kuwa ni Lilian Maraule , Glory Gideon, Melody Tryphone, Anitha Mlay, Silvia Mkomwa, Rogathe Ally, Prisca Dastan ambao wote wanatoka Dar es Salaam.
Warembo wengine ni Maureen Foster na Mary Peter wanaotoka Mwanza wakati anayetoka mkoa wa Mbeya ni Zahra Abdul.
Alisema kuwa warembo hao watakuwa chini ya Miss Universe namba mbili wa mwaka jana, Lilian Loth katika kambi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na SeaCliff Court Residence, Diana Magese, MnM, Kasakana na Bonuzi.
“Maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na wapenzi wa masuala ya urembo watapata burudani safi kutoka kwa DDI Dance, poetry group (Romantic), A beautiful song kutoka kwa Jeff Mduma,” alisema Maria.
Alifafanua kuwa wamedhamilia kumpata mrembo bora ambaye atarejesha heshima ya mashindano hayo kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata ambaye alimaliza katika nafasi tano bora nchini Mexico mwaka 2007.
“Tumefanya uchaguzi wa warembo vizuri na wengi ni bora, kwa sasa tunawafundisha masuala mbalimbali ya urembo, lengo ni kuwafanya wawe bora, wote ni washindi, lakini tunahitaji mshindi mmoja ambaye ataliwakilisha Taifa katika mashindano ya Kimataifa,” alisema.
Alisema kuwa mashindano hayo pia yatamtoa mshindi wa taji la Miss Earth Tanzania na mshindi wa taji la Miss Tourism Queen International wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.