Habari za Punde

SIMBA YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI YAIPA NJOMBE MJI 4-0 MUZAMIRU APIGA 2 NDANI YA DAKIKA 2

 Beki wa timu ya Simba Sc, Mohamed Hussein 'Tshabalala' akiruka kukwepa kwanja la beki wa Njombe Mji, Agaton Mapunda (chini) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Katika mchezo huo SImba wameshinda mabao 4-0 yaliyofungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya 27, Mzamiru Yassin dakika ya 51 na 52 na Laudit Mavugo dakika ya 58. 

TOP FOR LIGI KUU BARA
Simba sasa wamekaa kileleni wakiwa na jumla ya Pointi 15 na mabao 15 ya kufunga , nafasi ya pili akibaki Mtibwa Sugar akiwa na Pointi 15 na mabao 8 ya kufunga, nafasi ya tatu Azam Fc akiwa na Pointi 13 na mabao 5 ya kufunga, nafasi ya Nne Yanga Sc wakiwa na Pointi 12 na mabao 6 ya kufunga.

MATOKEO MENGINE YA MECHI ZA LIGI KUU LEO
Mtibwa Sugar 1- Tanzania Prisons 0
Mbao Fc 0 - Azam Fc 0
Lipuli Fc 1 - Majimaji 0
Mbeya City 2 - Ruvu Shooting 0
Ndanda Fc 0 - Singida Utd 0
Simba 4 - Njombe Mji 0
 Kiungo wa Simba SC, Mzamiru Yassin, akimtoka beki wa Njombe Mji, Laban Kambole, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
 Kipa wa Njombe Mji, Rajab Mbululo, akilala kuokoa hekaheka langoni kwake huku Nicholas Gyan, akijaribu kupiga mpira mbele wa beki Ahmed Adiwale. 
 Haruna Niyonzima (katikati) akijaribu kupenya katikati ya mabeki wa Njombe Mji.Ditram Nchimbi (kushoto) na Agaton Mapunda
 Kipa wa Njombe Mji, David Kissu, akiokoa shuti lililopigwa langoni kwake
 Laudit Mavugo (katikati) akijaribu kupenya katikati ya wachezaji wa Njombe Mji Claide Wigenge (kushoto) na Ahmed Adiwale.
 Emmanuel Okwi akimfinya beki wa Njombe Mji.....
  Emmanuel Okwi, akijiandaa kupiga shuti mbele ya Beki wa Njombe Mji, Laban Kambole, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
 Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi, akimtoka Beki wa Njombe Mji, Laban Kambole, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
 Mahmbuliaji wa Simba SC, Laudit Mavugo (kushoto) akijaribu kumhadaa beki wa Njombe Mji, Laban Kambole, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
 Beki wa timu ya Njombe Mji, Agaton Mapunda (kushoto) akichuana kuwania mpira na Kiungo wa Simba, Shizya Kichuya, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
 Shizya Kichuya, akimtoka beki wa Njombe Mji, Agaton Mapunda (kushoto) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.