Habari za Punde

STARS WAJIFUA 'NGANGARI' KUWASUBIRI MALAWI KESHOKUTWA

Mshambuliaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta akipiga mpira kumfunga kipa wa Stars, Aishi Manula. wakati wa mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterans.
  Wachezaji wa Kimataifa Mbwana Samatta ( wapili kulia) na Simon Msuva, wakiteta na kuonyeshana jambo wakati wa mazoezi ya pamoja ya timu ya Taifa, Taifa Stars katika Uwanja wa Boko Veterans, kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi unaotarajia kuchezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru.
 Mshambuliaji wa kimataifa wa Taifa Stars, Mbwana Samatta (katikati) akijaribu kuwatoka Mbaraka Yusuph, (kushoto) na Mohamed Issa, wakati wa mazoezi hayo.
Mshambuliaji wa Stars, Ramadhan Kichuya, akiwania mpira na beki Kelvin Yondan, wakati wa mazoezi hayo.
 Beki wa Stars, Gadiel Michael (kushoto) akipiga hesabu za kumtoka Erasto Nyoni, wakati wa mazoezi hayo.
 Msuva, akiwa mazoezini.....akijiandaa kupiga mpira....
Wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars, wakiwa katika mazoezi ya pamoja kwenye Uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars, wakiwa katika mazoezi ya pamoja kwenye Uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazoezi yao katika Uwanja wa Boko Veterans.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.