Habari za Punde

TAIFA STARS PUNGUFU YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA MALAWI KAMILI NYUMBANI

Na Tima Sikilo, Dar
TIMU ya Taifa Taifa Stars leo imeshindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam,Stars wakiwa pungufu wachezaji wawili.
Katika mchezo huo uliokuwa na kasi na kushambuliana kwa zamu ulikuwa wa kuvutia kutokana na kila timu kucheza kwa kujihami.
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Simon Msuva,  alikosa bao katika dakika ya 26, baada ya kutanguliziwa mpira mrefu na kubaki yeye na kipa aliyewahi na kuudaka shuti la Msuva lililomfanya kipa huyo kuumia.
Malawi ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Nahodha wake buliaji wake,Ngambi Robert katika dakika ya 36.
Dakika ya 53 Taifa Stars walifanya mabadiliko akitoka Raphael Daudi na kuingia Mbaraka Yusuph na dakika nne baadaye yakaonekana matunda ya mabadiko hayo ambapo Mbaraka Yusuph aliisawazishia Stars akimalizia pasi nzuri kutoka kwa Simon Msuva.
Dakika ya 65 Mbwana Samatta alikosa bao baada ya shuti lake kugonga mwamba, wakati samata akijaribu kumalizia pasi ya Erasto Nyoni.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Kocha wa Malawi aliwashangaza mashabiki waliohudhuria mchezp huo baada ya kuhama kutoka katika Benchi lake na kwenda katika benchi la Stars haikujulikana alikuwa akifuata nini, jambo ambalo lilimfanya mwamuzi wa mchezo huo kumpa kadi na iliyomuamuru kwenda jukwaani.
Taifa Stars walifanya mabadikiko mengine katika dakika ya 83 akitoka Simon Msuva na kuingia Abdul Hilal, anayekipiga na timu ya Tusker ya Kenya. Dakika ya 85 Beki wa Stars, Erasto Nyoni, alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Malawi.
Naye Muzamiru Yassin alizawadiwa kadi nyekundu katika dakika za nyongeza baada ya kumchezea rafu,Phiri Gerald, hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza kipyenga kuashiria kumalizika dakika 90 mabao yalikuwa Tanzania Taifa Stars 1- Malawi 1.

1 comment:

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.