Habari za Punde

TANZANIA YATWAA TAJI LA CANA KANDA YA TATU KWA MARA YA PILI MFULULIZO KUOGELEA

 Makocha wa timu ya Tanzania wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu kwa mchezo wa kuogele leo
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akimkabidhi kombe Nahodha wa Tanzania, Sonia Tumiotto pamoja na Natalie Sanford baada ya kutwaa ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu.
 Waogeleaji wa timu ya Tanzania  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutetea vyema ubingwa wa Cana kanda ya tatu.
Baadhi ya mashabiki wa mchezo wa kuogelea hapo wakishangilia kwa nguvu kuwapa hamasa waogeleaji katika mashindano ya 'relay'.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha kuogelea (TSA), Thauriya Diria (kushoto) na Katibu Mkuu wake, Ramadhan Namkoveka wakiwa katika pozi la 'ushindi' baada ya Tanzania kutangazwa kutetea ubingwa wa Kanda ya tatu wa Cana.
 Muogeaji nyota wa Tanzania, Sonia Tumiotto akipigania Taifa lake katika mashindano ya Cana kanda ya tatu.
Collins Saliboko wa Tanzania akishindana katika mashindano ya Cana Kanda ya Tatu Afrika.
*********************************************************
Na Ripota wa Mafoto Bloga, Dar
Tanzania imefanikiwa kutetea ubingwa wa Cana Kanda ya Tatu Afrika baada ya kuibuka katika nafasi ya kwanza katika upande wa wanawake na wanaume.
Kwa mujibu wa matokeo  yaliyotangazwa juzi, timu ya Tanzania ilipata jumla ya pointi 1,394 na kufanikiwa kuzishinda timu maarufu na kali katika mchezo huo, Zambia ambayo ilipata pointi 968 na Kenya iliyomaliza ya tatu kwa pointi 957.
Uganda ambayo ndiyo nchi ya kwanza kuandaa mashindano hayo, ilimaliza ya nne kwa kupata pointi 759 na kufuatiwa na Afrika Kusini iliyopata pointi 469 ma Sudani iliyopata oint 459 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux, Coca Cola, Label Promotions, Tanzania Sign Writers, Giraffe Ocean View, Print Galore na Slipway Hotel.
Katika mashindano hayo ya siku tatu, timu ya wanawake wa Tanzania ndiyo ilikuwa kali zaidi kutokana na kuundwa na waogeleaji nyokta kama Sonia Tumiotto ambaye ndiye nahodha na Natalie Sanford. Mbali ya hao kulikuwa na nyota wengine kama Maia Tumiotto ambaye anakuja juu kwa kasi, Smriti Gorkan, Kayla Gouws, Amani Doggart,  Tara Behnsen, Emma Imhoff, Rania Karume , Chichi Zengeni,  Anjani Taylor, Anna Guild, Sanne Kleinveld ,  Angelica Spence, na Tami Triller.
Kwa upande wa wanaume , nyota alikuwa Marin De Villard pamoja na wakali wengine kama  Collins Saliboko, Joseph Sumari, Denis Mhini,  Hilal Hilal, Adil Bharmal, Judah Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick, Caleb O'Sullivan, Khaleed Ladha, Matthew Guild ,  Chris Fitzpatrick, Harry McIntosh, Dhashrrad Magesvaran na  Joseph Sumari.
 Kwa upande wa timu ya Platnum, nayo ilionyesha kuwa kuna nyota wa baadaye wa Tanzania ambapo timu ya wanawake iliindwa na  Shivan Bhatt, Natalia, Charlotte Sanford,  Vanessa Dickson ), Rebecca Guild, Meredith Boo , Maria Bachmann ), Kayla Temba na  Maya Somaiya.
Kwa wanaume walikuwa Aravind Raghavendran, Mohameduwais Abdullatif (Bluefins), Abraham Kayugwa, Terry Tarimo,  Aliasgar Chakera, Zeke Boos , Yuki Omari, Augustino Lucas , Fallih Ahmed,  Carter Helsby ,  Ian Lukaza na Emmanuel Stenson.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza aliwapongeza waogeleaji wa Tanzania kwa kutwaa ubingwa huo huku akiahidi kutoa ushirikiano mkubwa  kwa chama cha kuogelea cha Tanzania (TSA).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.