Habari za Punde

TFF WAKANUSHA TAARIFA ZA UWANJA WA TAIFA KUTUMIKA OKT 28 YANGA NA SIMBA

Uwanja wa Taifa ukiwa katika hatua za mwisho za marekebisho baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kupisha marekebisho ya uwanja huo eneo la kuchezea 'Pitch' ambalo limeoteshwa nyasi mpya na kuondolewa zile zilizokuwa zimepandwa kwa muda wakati wa mechi ya Everton. 
Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara wa Watani wa Jadi Yanga na Simba ni matarajio ya wengi kwamba wahusika wangetumia busara tu kuruhusu mchezo huo kupigwa katika uwanja huu badala ya ule wa Uhuru ambao unaokenaka utakuwa ni kero na hasa kwa mcheo mkubwa wa watani wa jadi.
Mbali na mashabiki wa soka kuanza kuudisi uwanja huo kutumika kwa mechi kubwa kama hiyo lakini hata timu husika zenyewe zimekuwa zikiimba TFF kuhamisha mchezo huo kama wenyeji Yanga walivyoomba kuhamishia kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na kukataliwa na Shirikisho ambao wameendelea kushikilia msimamo wao mchezo kupigwa Uhuru.
Leo TFF wamekanusha kuhusu tetesi za wao kurusu mchezo huo kupigwa katika uwanja huu wakishikilia msimamo wao kuwa mchezo utapigwa katika Uwanja wa Uhuru kama walivyotangaza awali.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.