Habari za Punde

VIJANA JIUNGENI NA VIKUNDI VYA MAZOEZI: NAIBU WAZIRI SHONZA

  Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza  (mwenye tisheti nyeupe  katikati) akiwa katika mazoezi ya jogging  na kikundi cha Kawe Jogging Social Club katika sherehe za miaka mitano ya kikundi hicho  zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam (aliyenyoosha kidole  kushoto) ni Katibu wa Kawe Jogging Social Club Bw.Alhaj Seif Muhere.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza  (mwenye tisheti nyeupe  katikati)akifanya mazoezi ya viungo na wanachama wa vikundi mbalimbali vya jogging mkoani Dar es Salaam katika sherehe za miaka mitano ya kikundi cha Kawe Jogging Social Club leo,(kushoto)  Katibu wa Kawe Jogging Social Club Bw.Alhaj Seif Muhere na kulia ni Mwanachama wa Jogging Kawe Social Club Bi Felister Mwijage. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza  akizungumza na wanachama  wa vikundi mbalimbali vya jogging Mkoani Dar es Salaam katika sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya kikundi cha Kawe Jogging Social Club zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam.
****************************************
Na Anitha Jonas – WHUSM
Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni  Sanaa na Michezo  Mhe. Juliana Shonza ametoa  wito kwa vijana  kujiunga na vikundi vya mazoezi maarufu kama (Jogging Club) kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kujikwamua kiuchumi.
Mheshimiwa  Naibu Waziri  ametoa wito huo katika sherehe za maadhimisho ya  miaka mitano ya Kawe Jogging Social Club zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo aliwapongeza wanachama wa Klabu hiyo kwa kuweza kudumu kwa muda  wote huo.
“Napenda kuwapongeza kwa juhudi zenu pamoja na ubunifu mliyoutumia katika kujiongezea kipato kupitia klabu yenu kwa kuanzisha mgahawa ambao unawaongezea kipato na kukuza uchumi wenu kwa hakika mmekuwa ni mfano wa kuigwa,”Mhe. Shonza.
Akiendelea kuzungumza katika sherehe hizo Naibu Waziri huyo amewahakikishia wanaklabu hao ushirikiano pamoja na kushughulikia maombi yao ya kupatiwa mashine ya maximalipo.
Naye Mwenyekiti wa Kawe Jogging  Social Club  Bw. Abdul Risasi alimshukuru Naibu Waziri kwa kujumuika nao katika sherehe hiyo na kutoa ombi la kusaidiwa kupata mfadhili atakayeweza kuwasaidia kufanikisha ushiriki wao katika mashindano ya Kilimarathon yanayotarajia kufanyika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
“Tumekuwa tunashiriki katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon kwa miaka minne mpaka sasa na Kawe Jogging Social Club imekuwa ndiyo kikundi pekee nchi nzima  ambacho kimepata nafasi ya kuweza kushiriki mashindano hayo ambapo wanachama wake hukimbia mpaka kilometa 21,”alisema Bw.Risasi.
Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo aliendelea kutoa wito kwa vijana kujiunga katika vikundi vya jogging kwani kupitia umoja huo wanaweza kujitengeneza fursa za kiuchumi na kujiongezea kipato badala ya kukaa vijiweni na kulalamikia hali ngumu ya maisha.
Kwa upande wa mmoja wa wanachama wa Msasani Jogging Club Bi Asha Said alitoa maoni yake na kusema jogging clubs ni nzuri kwani zinasaidia kupata marafiki pamoja na kuimarisha afya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.