Habari za Punde

WATU WATANO WAFARIKI AJALI YA ROLI NA HIACE MULEBA

Watu watano wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace kugongana na lori kisha kuwaka moto.
Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Kyamyorwa wilayani Muleba mkoani Kagera. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Oktoba 20, saa 12:00 asubuhi.
Amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo.
Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliokufa, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo, kondakta na abiria watatu.
Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka. Picha kwa Hisani ya BukobaWadau Blog

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.