Habari za Punde

WAZIRI DKT KALEMANI AANZA ZIARA KUKAGUA KITUO CHA UDHIBITI WA UMEME

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefika Dar es Salaam asbuhi hii akitokea Dodoma kwa ajili ya kukagua mitambo ya Umeme na mifumo ya Umeme ili kuweza kurudisha Umeme katika Gridi ya Taifa ambayo ilipata hitilafu jana saa 12: 30 jioni na kusababisha baadhi ya mikoa kukosa Umeme.
Ameanza ziara kwa kukagua kituo cha udhibiti wa mifumo ya Umeme cha Ubungo na kisha kuelekea katika mitambo ya kuzalisha Umeme ya Kinyerezi I jijini Dar es Salaam (MW 150).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.