Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MBIO ZA KILI MARATHON ZA 2018

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Mbio za Kili Marathon 2018 zinazotarajia kufanyika mwezi Machi mwakani mkoani Kilimanjaro, uzinduzi huo umefanyika leo kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Masoko wa TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt, Warda Kimaro, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Henry Kinabo, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, (wa nne kutoka kulia) ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Alex Mkanyenge (kushoto kwa Waziri) ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli (wa pili kulia) ni Mkurugenzi Masoko wa TBL, Thomas Kamphuis na Makamu wa Rais wa AT, William Kallage. 
 Mbio za Kili Marathon 2018 zimezinduliwa rasmi
 Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi mbio za Kili  Marathon zinazotarajia kutimua vumbi Machi 4, mwakani Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mbio hizo zinazofanyika mfululizo mwaka wa 16 zinatarajia kushirikisha zaidi ya wakimbiaji 30,000 kutoka nchi mbalimbali duniani, ambapo mshindi wa kwanza wa kilomita 42 atajinyakulia shilingi milioni nne taslimu.
Mbio hizo za 16 ambazo zinafanyika kila mwaka tangu zilipoanza mwaka 2003, zinatarajia kuiingizia mapato nchi kutokana na mamia ya wageni wanaokuja kushiriki kutoka nje ya nchi.
Akizindua mbio hizo, WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Mwakyembe amesema Kilimanjaro Marathon imejizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa maandalizi yake ni mazuri na kuwataka waandaaji wa mbio nyingine kuiga mfano huo.
“Tunataka kuwaibua kina Felix Simbu wengine na hili linawezekana tu kupitia mbio kubwa kama Kilimanjaro Marathon. 
Nimefahamishwa kuwa Simbu pia alitokana na mbio hizi kwani aliwahi kushiriki kilometa 21 miaka ya nyuma, sisi kama serikali tutafanya kila linalowezekana kuyafikia malengo haya,” alisema Dkt. Mwakyembe.
Alisema uwepo wa mashindano hayo utasaidia nchi kupata mapato katika nyanja ya utalii kutokana na washiriki wengi wanatoka nje ya nchi kwa ajili ya kuchuana na watanzania.
Dkt. Mwakyembe alisema mashindano hayo yatasaidia kupata wanariadha watakaofuzu vigezo kwa ajili ya kuchuana katika mbio za kimataifa ikiwemo za Afrika Mashariki na Kati kwa kuwa mbio hizo zimesajiliwa na Shirikisho la Riadha cha Kimataifa (IAAF).
Naye Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis, alisema wanajivunia kudhamini mbio hizo kwa miaka 16 kutokana na ukuaji kwa kasi kubwa mwaka hadi mwaka.
Tigo nayo inadhamini mbio hizo katika michuano ya kilometa 21. Mshindi wa kwanza wa kilomita 21 kwa upande wa wanaume na wakike watajinyakulia milioni 2 kila mmoja wa pili milioni 1 wakati wa tatu watapata 650,000.
 Baadhi ya wadau na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
 Mwendesha Shughuli Agrey Mareale akisimamia shoo....
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.