Habari za Punde

WAZIRI UMMY MWALIMU AIPIGA TAFU TIMU YA AFRICAN SPORTS

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akimkabidhi Nahodha wa timu ya African Sports hundi ya sh milioni 2.1,
***************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameikabidhi timu ya African Sports sh. milioni mbili kwa ajili ya posho za wachezaji na maandalizi ya michezo ya igi daraja la pili Tanzania Bara (SDL).
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Ummy alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuiwezesha timu hiyo kutimiza adhima ya kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
 Alisema timu hiyo ikipanda katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara itasaidia kuongeza mapato katika jiji la Tanga kutokana na viingilio vya mashabiki uwanjani.
Ummy aliitaka timu hiyo ihakikishe inafanya vyema katika michuano hiyo ili kuweza kurejesha hadhi yake ya miaka ya nyuma katika medani ya soka nchini.
Mbali na msaada huo, waziri huyo ameilipia timu hiyo 500,000 kama ada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya Leseni za wachezaji.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.