Habari za Punde

YANGA YAANZA KUWAJIBU WATANI, AJIBU APIGA 2 WAKIICHAPA STAND UNITED 4-0

 Kiungo wa Yanga, Ibrahim Ajib akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Katika mchezo huo Yanga wameshinda mabao 4-0.
*************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Shinyanga
KAZI nzuri iliyofanywa na kiungo wa Yanga, Ibrahimu Ajib Migomba katika dakika ya 24 na 30 imetosha kuwavunja nguvu Stand United na kuwahakikishia ushindi mnono watetezi wa Ubingwa wa Ligi Kuu Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa kambaragemjini Shinyanga jioni ya leo.
Kwa ushindi huo wa Yanga wa mabao 4-0 unaamsha shambrashambra za mchezo wa watani wa Jadi Yanga na Simba unaotarajia kpigwa Okt 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, baada ya Simba jana kuibuka na ushindi kama huo dhidi ya Njombe Mji huku Yanga nao leo wakifanya hivyo dhidi ya Stand United.

Pius Buswita akishangilia bao lake.....
 Wachezaji wa Yanga wakipongeza Pius Buswita baada ya kufunga bao la tatu kati ya manne leo.
************************************************
Katika mchezo wa leo Yanga walinekana kutulia zaidi huku wakicheza kama wenyeji wa uwanja na kushambulia kwa kasi muda wote jambo lililowafanya Stand kushindwa kujiamini na kufanya papara kila walipofika katika lango la wapinzani.
Ibrahim Hajib Migomba, alifungua pazia la mabao ya Yanga katika dakika ya 24 kwa mpira wa adhabu baada ya Geofrey Mwashiuya kuchezewa rafu nje kidogo ya 18 na dakika sita baadaye alifanya kazi nzuri kwa kumalizia pasi nzuri ya Obrey Chirwa aliyepambana na kuwatoka mabeki wawili wa Stand United na kisha kupiga Krosi fupi ya chini iliyomkuta Ajibu na kufunga bao la pili akiwa katikati ya mabeki wawili.
 Buswita (kushoto) akimpongeza Chirwa baada ya kufunga bao la Nne.... 
Yusuf Mhilu akichuana kuwania mpira na beki wa Stand United.
****************************************
Bao la tatu lilifungwa na Kiungo Kiungo Pius Buswita katika dakika ya 53 akimalizia mpira wa kona iliyopigwa na Geofrey Mwashiuya na bao la kufunga pazia la mabao lilifungwa na Obrey Chirwa katika dakika ya 69 akiitendea haki pasi nzuri ndefu ya Pius Buswita, ambapo amzidi mbio beki na kupishana na kipa wa Stand kisha kuukwamisha wavuni mpira huo.
Baada ya mchezo wa leo Yanga sasa inafikisha pointi 15 sawa na watani wao Simba baada ya kucheza mechi saba na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa nyuma kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa na watani wao Simba SC ambao pia wana pointi 15 sawa na Mtibwa Sugar walio nafasi ya tatu. 
 Obrey Chirwa akichuana kuwania mpira na kipa wa Stand United na kufunga bao la Nne.
********************************************
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Erick Onoka kutoka Arusha aliyesaidiwa na Omary Juma na Vincent Mlabu, Stand United walikaribia kupata bao dakika ya kwanza tu baada ya shuti la mpira wa adhabu la Hamad Kibopile kumchomoka mikononi kipa Mcameroon wa Yanga, Youthe Rostand ambaye hata hivyo aligeuka haraka na kuukamata kabla haujavuka mstari.
Baada ya mchezo wa leo Yanga inatarajiwa kuelekea Visiwania Pemba kesho kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wao ujao dhidi ya Simba.
 Ibrahim Ajib, akijaribu kumtoka beki wa Stand United....
 Buswita akijiandaa kupiga krosi iliyozaa bao la Nne....
 Wachezaji wakimpongeza Ajib.....
 Beki wa Yanga Gadiel Michael (kulia) akijaaribu kumtoka mchezaji wa Stand United
 Geofrey Mwashiuya akimtoka beki wa Stand United
 Obrey Chirwa akichuana kuwania mpira na beki wa Stand
 Geofrey Mwashiuya (kulia) akimtoka beki wa Stand na kutengeneza faulo iliyozaa bao la kwanza.
Chirwa akimtoka beki wa Stand...
********************************************
KIKISI CHA STAND UNITED: Frank Muwonge/Mohammed Makaka dk73, Aaron Lulambo, Hamad Kibopile, Erick Mulilo, Ally Ally, Rajab Rashid, Ambros James/Morris Mahela dk67, John Mwitiko, Adam Salamba, Wisdom Mutasa na Emmanuel Kitoba/Bakari Mohammed dk42.

KIKOSI CHA YANGA SC: Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Pato Ngonyani, Pius Buswita, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa/Yussuf Mhilu dk77, Ibrahim Hajib/Mussa Said dk71 na Geoffrey Mwashiuya/Emmanuel Martin dk82.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.