Habari za Punde

AZAM FC YAMTEMA WA KIMATAIFA MMOJA NI YAHYA MOHAMED

KLABU ya Azam FC, le imetangaza rasmi kuachana na mshambuliaji wake wa kimatafa, kutoka Ghana, Yahya Mohammed,  baada ya makubaliano ya pande zote mbili kuridhiana.
Akizungumza na mtandao huu, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi, amesema  klabu hiyo imeamua kuachana na huduma ya mghana huyo aliyeisaidia timu katika michuano ya kombe la mapinduzi hadi kuwa Mabingwa watetezi, kutokana na kutoridhishwa na uwajibikaji wake kwenye timu (kushuka kiwango).
“Yalikuwa makubaliano baina yetu, baada ya sisi kama klabu kutoridhishwa na mchango wake kwetu, hivyo kuanzia sasa yuko huru,”amesema Jaffar.
Yahya alisajiliwa Azam FC kwa matarajio makubwa Juni mwaka jana kwa dau la dola za Kimarekani, 100,000 zaidi ya Sh. Milioni 220 kutoka Aduana Stars ya kwao.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji watano wa Ghana waliosajiliwa Azam FC wakati huo, wengine ni Daniel Amoah, Enoch Atta Agyei kutoka Medeama SC, Samuel Afful kutoka Sekondi Hasaacas na Yakubu Mohammed kutoka Aduana Stars pia.
Mwanzoni mwa msimu, Azam FC ilimtema Afful na kumsajili kipa Mghana, Razak Abalora kutoka klabu ya Wafa ya kwao. Jaffar amesema baada ya kuondolewa kwa Yahya, kocha Mromania, Aristica Cioaba amepewa jukumu la kusajili mshambuliaji mwingine.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.