Habari za Punde

BLUEFINS YASHIKA NAFASI YA PILI MASHINDANO YA KUOGELEA YA MOROGORO

 Waogeleaji wa Bluefins wakiwa katika picha ya pamoja na makocha na viongozi mara baada ya kuzawadiwa medali
 Waogeleaji wa klabu ya Bluefins wakipambana katika mashindano ya kuogelea ya Morogoro
Waogeleaji wa klabu ya Bluefins wakipambana katika mashindano ya kuogelea ya Morogoro
********************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Klabu  iliyoanzishwa miaka minne iliyopita ya ya mchezo wa kuogelea nchini, Bluefins imeanza kutamba baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano ya kuogelea ya Morogoro.
Klabu hiyo yenye makazi yake jijini, iliweza kujikusanyia pointi 3803 katika mashindano hayo ya siku tatu yaliyoshirikishaklabu mbalimbali kongwe nchini. Wenyeji wa mashindano hayo, Shule ya Kimataifa ya Morogoro (MIS) ilitwaa nafasi ya kwanza ambapo Dar Swim Club (DSC) ilimaliza katika nafasi ya tatu.
Blueifins ambayo ina waogeleaji chipukizi, iliweza kutwaa  jumla ya medali  103, 37 zikiwa ni dhahabu, 29 fedha na 37 shaba.
Mbali ya kushika nafasi ya pili, klabu hiyo pia iliweza kutoa washindi wawili wa jumla  kwa upande wa waogeleaji wa kiume kupitia kwa William Sereki ambaye ana umri wa miaka sita na vile vile kwa upande wa umri wa miaka nane ambapo Aminaz Kachra (msichana)  na Issac Mukani (mvulana) waliibuka washindi.
Muasisi na kocha wa timu hiyo, Rahim Alidina ushindi huo ni sishara tosha kuwa wanazidi kupata mafanikio makubwa katika mchezo wa kuogelea hapa nchini pamoja na kuwa na miaka minne tu katika mchezo na waogeaji wao wengi ni chipukizi.
“Mafundisho mazuri na moyo wa kujituma kutoka kwa wachezaji, makocha, viongozi na wazazi ndiyo nyenzo iliyotufikisha hapa, tulianza kwa kusua sua na tunashukuru klabu yetu kwa sasa ni miongoni mwa klabu zinazokuja juu kwa kasi katika mchezo huu,”
“Pia tuliweza kutoa waogeleaji wawili kwenye timu ya Taifa iliyotwaa ubingwa wa mashindano ya Cana ya Kanda ya tatu, waogeleaji wetu,  Aravind Raghavendran na  Mohameduwais Abdullatif walikuwa kwenye timu ya Taifa na kufanya vyema,” alisema Alidina.
Alisema kuwa hawata bweteka na mafanikio hayo na watazidi kufanya jitihada ili kuwa klabu namba moja nchini katika mchezo huo.
“Juhudi na ushirikiano wetu ndiyo umetifikisha hapa, hii ni chachu kwetu ya kuendelea kufanya vyema, lengoletu ni kuwa nafasi ya kwanza, tunaamini tutafikia lengo hilo,” alisema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.