Habari za Punde

EMMARSON MNANGAGWA AAPISHWA KUWA RAIS WA ZIMBABWE

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa akiapishwa rasmi leo kuwa Rais wa nchi hiyo baada ya kurejea nyumbani kutoka uhamishoni Jumatano wiki hii.  Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.
Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, kutangaza kuachia ngazi na kuacha madaraka hayo ya urais baada ya miaka 37 ya utawala wake wa kiimla. Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano wiki hii ameapishwa katika uwanja michezo wa Harare.
Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .
Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza "utamaduni wa ufisadi". Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 zilitangazwa siku ya Jumanne na kuibua shangwe kubwa katika mitaa mbalimbali ya nchini Zimbabwe.
Taarifa hiyo ilitolewa kwa njia ya barua na kutangazwa na Spika wa Bunge la nchi hiyo na kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae kikakatizwa.
Katika barua hiyo Rais Mugabe alisema anajiuzulu ili kuruhusu mchakato rahisi na wa amani wa ukabidhianaji mamlaka na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa hiyari.Rais Mugabe alishutumiwa kwa kumuandaa mkewe Grace kuchukua wadhfa wa urais, hata hivyo Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu Jumapili, na hawajatokea katika sherehe hizo za kuapishwa na haifahamiki wako wapi .
Alhamis , taarifa zilielezea kuwa Mugabe amepewa kinga ya kutoshtakiwa.
Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa michezo mjini Harare wenye viti 60,000- huku waandalizi wakiwataka Wazimbabwe kuhudhuria kwa wingi sherehe hizo.
lhamisi Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini (MDC ) alitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi makubwa ya kisiasa ili kuondoa masuala yaliyoweka madarakani kwa muda mrefu utawala wa Mugabe.Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement fo Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai.
************************************************
Munangagwa alikimbilia nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita- na kurejea nchini Jumatano wiki hii nakupokelewa kama shujaa.
Mnangagwa aliahidi kubuni ajira ambapo baadhi wanakadiria kuwa 90% ya watu hawana ajira.
"Tunataka kukuza uchumi wetu, tunataka amani, tunataka kazi, kazi, kazi ," aliuambia umati wa watu uliomshangilia mjini Harare.
Jumatano chama tawala cha ZANU PF kilisema kitafanya mageuzi kuondoa sheria zilizomfanya Mugabe kuwepo madarakani kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.