Habari za Punde

KITILYA, MASHA, MSENDO, KATAMBI WAJIUNGA CCM, KAMATI YARIDHIA KUMSAMEHE SOFIA SIMBA AREJEE KUNDINI

 Wanachama wapya wa CCM waliopokelewa wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM leo Ikulu jijini Dar es Salaam, wakiwa katika kikao hicho. Kutoka kushoto ni Albert Msendo, (aliyekuwa Mwanasheria wa ACT Wazalendo, Samson Mwigamba (ACT Wazalendo),  Patrobac Katambi (aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA Taifa BAVICHA), Edna Sanga (ACT Wazalendo), Lawrance Masha (CHADEMA) na Kitilya Mkumbo (ACT Wazalendo). Katika Kikao hicho Mwenyekiti Dtk Magufuli, alisoma hadharani barua ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Sofia Simba, aliyoandika mara kadhaa kuomba asamehewe na wajumbe wakaridhia kwa pamoja kumsamehe na kutangazwa kuruhusiwa kurejea kundini
 Hapa ni wakati wakiwasili ukumbini hapo katika Kikao hicho leo kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wajumbe wa Kamati ya Halmashauri Kuu CCM kujiunga nao.
 Mwenyekiti  wa Chama cha Mapinduzi CCM, John Pombe Magufuli, akifungua Kikao cha Halmashauri Kuu kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakiteta jambo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhman Kinana (kushoto) na  wakifuatilia kikao hicho.
 Wajumbe wakijadili jambo
 Wajumbe wakifuatilia kinachoendelea ukumbini hapo
 Mbunge wa Mtama Nape Nnauye (kulia) na Mbunge wa Bumbuli, Januri Makamba, wakifuatilia kikao hicho. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

 Viongozi wakuu ndani ya kikao hicho
 Wajumbe wakifurahia kwa kupiga makofi kupongeza maamuzi ya wanachama wapya hao kujiunga na CCM.
 Mwenyekiti wa  CCM, Rais Dk. John Magufuli, akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Ikulu, Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. 
 Kitilya Mkumbo, akiomba ridhaa ya kujiunga na CCM
 Rawrance Masha, akiomba ridhaa ya kurejea na kujiunga na CCM
 Samson Mwigamba, ACT Wazalendo, akiomba ridhaa kujiunga na CCM
 Mwanasheria wa chama cha ACT Wazalendo, Albert Msendo, akiomba ridhaa ya wajumbe wa NEC kujiunga CCM
 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA Taifa (BAVICHA)  Patrobac Katambi, akiomba ridhaa ya wajumbe hao kujiunga CCM.
 Musendo akishukuru kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Magufuli
Katambi, akishukuru kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Magufuli
 Wanachama wapya wa CCM wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 Wanachama wapya wa CCM wakipiga picha ya kumbukumbu na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Polepole.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.