Habari za Punde

KOCHA MAYANGA AFANYA MABADILIKO KIKOSI CHA TAIFA STARS

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga amewaita kikosini viungo Jonas Mkude kutoka Simba na Mudathir Yahya wa Singida United.
Mkude na Mudathir wanachukuwa nafasi za Erasto Nyoni na Muzamiru Yassin wote kutoka Simba ambao awali walijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 walioitwa na Mayanga.
Kocha Mayanga amelazimika kuwaondoa kikosini Nyoni na Muzamiru baada ya taarifa ya ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusiana na kadi nyekundu walizopata wachezaji hao kwenye mchezo wa kirafiki uliopita.
Mchezo uliopita ulikuwa ni dhidi ya timu ya The Flames ya Malawi uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa FIFA, Nyoni na Muzamiru wataukosa mchezo ujao dhidi ya Benin kutokana na Kanuni za Nidhamu za FIFA ambako kifungu cha 18 (4) kinaelekeza mchezaji mwenye kadi nyekundu kuukosa mchezo unaofuata.
Kwa suala la mechi za kirafiki kifungu cha 38 (2) (g), kinatamka wazi kuwa mchezaji mwenye adhabu ya kadi nyekundu moja kwa moja anaukosa mchezo wa kirafiki unaofuata.
Kwa ufafanuzi huo wa FIFA, Mayanga amewaondoa Nyoni na Muzamiru kikosini ili kutumikia adhabu hiyo kwa mchezo unaofuata wa kirafiki na nafasi zao kujazwa na Mkude na Mudathir.
Wachezaji hao watajiunga kambini na wachezaji wengine walioitwa katika kambi itakayoanza Novemba 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Benin utakaochezwa kwenye tarehe za kwenye kalenda ya FIFA Novemba 12, huko Benin.
Wachezaji wengine wanaounda kikosi hicho kinachodhaminiwa na Bia ya Serengeti ni:- 

MAKIPA: –

1. Aishi Manula
2. Ramadhani Kabwili
3. Peter Manyika

WALINZI WA PEMBENI:- 
4. Gadiel Michael
5. Boniphas Maganga

WALINZI WA KATI
6. Abdi Banda
7. Kelvin Yondani
8. Nurdin Chona
9. Dickson Job

VIUNGO WA KATI:- 
10. Himid Mao
11. Hamis Abdallah
12. Raphael Daudi
13. Mohamed Issa

VIUNGO WA PEMBENI:- 
14. Simon Msuva
15. Shiza Kichuya
16. Faridi Mussa
17. Ibrahim Ajib

WASHAMBULIAJI:- 
18. Mbwana Samatta
19. Mbaraka Yusuph
20. Elias Maguli
21. Yohana Mkomola
22. Abdul Mohamed

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.