Habari za Punde

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KALETENI MABADILIKO KATIKA MAENEO YENU: KATIBU MKUU SIHABA NKINGA

 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii Bibi. Sihaba Nkinga  katika Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaomalizika leo Mjini Dodoma na kuwasisitiza kwenda kuleta mabadiliko sehemu walizopo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
 ***********************************
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kwenda kuleta mabadiliko katika maeneo yao.
Ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati wa Siku ya mwisho ya Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo unaomalizika leo mjini Dodoma na kusisitiza kuwa wao ni watu muhimu na wanayodhamana ya kuleta mabadiliko katika maeneo yao kwa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo jumuishi na endelevu.
Ameongeza kuwa ubunifu na uwajibikaji kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ni tunu kubwa itakayowezesha wawezesha kuwa chachu ya mabadiliko katika maeneo mnayotumika jamii.
“Niwaombe Maafisa Maendeleo ya Jamii mliopo hapa na muwafikishie ujumbe wasiokuwepo katika Mkutano huu kuwa wanatakiwa kuwa chachu ya mabadiliko katika maeneo yao” alisema Bibi. Sihaba.
Aidha, Bibi Sihaba Nkinga amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kama wasajili wasaidizi wa Mashirika Yasiyokuwa ya Serikali kuwajibu wa kuonesha uzalendo na utanzania wetu kwa kuhakikisha kuwa mashirika (NGOs) yanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na Kanuni ili kutoa mchango katika sekta zinazosisimua ukuaji wa maendeleo ya nchi na kusisimua ustawi wa jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba amewashauri Maafisa Maendeleo ya Jamii kuzingatia Kanuni na Sheria katika kuratibu ufanyaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika maeneo yao.
“Tuzingatie Sheria na Kanuni katika kuyaratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika maeneo yetu” alisema Bw. Katemba
Naye kwa niaba ya Maafisa Maendeleo ya Jamii Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kyela  Bi. Nelusigwa Mwakigonja ameishukuru Wizara mama kwa kuwaleta pamoja Maafisa Maendeleo ya Jamii na kutoa maelekezo kwao ili waweze kuleta mabadiliko katika sehemu zao za kazi.
“Tunaishukuru Wizara kwa kutuleta pamoja na tunaahidi tutaenda kuyatekeleza maelekezo yote tuliyoyapata kutoka kwa viongozi wetu” alisema Bi Nelusigwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.